Wananchi wa kata ya Itumbili iliyopo Wilaya ya Magu mkoa wa Mwanza ,wamemuomba Rais John Pombe Magufuli na serikali yake ya awamu ya tano kuwaondoa madiwani mizigo wanaopeperusha bendera ya chama cha mapinduzi kwenye uchaguzi mkuu ujao wa 2020 kwakua madiwani hao  hawaendani na kasi ya Rais Magufuli.


Aidha kwa nyakati tofauti,wananchi hao walitoa kilio chao kwa diwani wa kata yao Issack Malaki Lupondije ambako wanadai licha ya kuwa diwani kijana na mdogo zaidi wilayani Magu ameshindwa kuendana na kasi ya maendeleo anayoyafanya Rais Magufuli na badala yake amejeuka kuwa diwani mtalii ambaye anaishi mkoa wa Dar es salaam na sio kwenye kata yake anayoiongoza kama diwani.  

Wananchi hao waliendelea kueleza kuwa  diwani huyo amekua akionekana kwa nadra kwenye kata yake,na ameshindwa kusimamia maendeleo ya miradi mbalimbali iliyoletwa na serikali ya awamu ya tano inayotekelezwa kwenye kata yake, hata tu kukaa vikao vya WODC kwakwe imekua ni kazi.

“Mfano mwananchi akimtafuta anamwambia atumie Facebook na WhatsApp kumpata na  malalamiko na shida zake sasa sisi wananchi tena tupo kijijini tutapataje hizo simu ili tuweze kuwasiliana na diwani wetu,”alisema mwananchi 

“Sisi tunasikia hana kazi zaidi ya kutapeli na tayari analalamikiwa na viongozi wa chama cha mapinduzi akiwemo Mwenyekiti wa Ccm wa wilaya hata kudiriki kutembea na kitambulisho cha  mwenyekiti wa Halmashauri ya Magu Elisha Hillary kufanya utapeli, sisi tunaumia kwakua tulimchagua yeye na tulimpa kazi ya kutuongoza,hivyo anachofanya ni ametusaliti sisi kama wananchi wanyonge maana hatukumtuma kufanya hicho anachokifanya,alisema  mwananchi huyo 

“Tunaona vijana wenzake wakifanya vizuri sana,yeye hatupi fursa hiyo ila tunasikia kuwa yeye anapenda kulelewa na wanawake sasa hii imetuchosha,kwakua tunamuunga mkono Rais Magufuli basi chama cha mapinduzi kisimamie ilani yake vyema na kutuletea viongozi wenye nia kama ya Rais John Pombe Magufuli kusaidia wananchi na si kupata nafasi ya kwaajili ya masilahi yao binafsi“.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: