Wednesday, 11 March 2020

TCDC YATOA MAFUNZO KWA VIONGOZI WA SACCOS JIJINI DAR ES SALAAM KUHUSU SHERIA YA HUDUMA NDOGO ZA KIFEDHA


Mrajis Msaidizi anayesimamia Vyama vya Ushirika wa Kifedha kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC), Josephat Kisamalala, akizungumza katika mafunzo ya siku mbili kwa viongozi na watendaji SACCOS Mkoa wa Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Katibu wa Movenpick Royal Palm SACCOS, Abiel Mkongwa, Mrajis Mkoa wa Dar es Salaam, Abdillahi Mutabazi, Naibu Mrajis wa Vyama vya Ushirika, Collins Nyakunga na Katibu Tawala Msaidizi sehemu ya uchumi na uzalishaji Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Elizabeth Mshote.
Katibu Tawala Msaidizi sehemu ya uchumi na uzalishaji Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Elizabeth Mshote, akizungumza katika mafunzo hayo.
Washiriki wa mafunzo hayo.
Naibu Mrajis wa Vyama vya Ushirika, Collins Nyakunga, akifungua mafunzo hayo.
Washiriki wa mafunzo hayo. Mrajis Mkoa wa Dar es Salaam, Mutabazi, akizungumza katika mafunzo hayo.
Washiriki wa mafunzo hayo.
Washiriki wa mafunzo hayo.
Mwanasheria wa Tume ya Maendeleo  ya Ushirika Tanzania (TCDC),  Shani Mayosa, akitoa mada.
Katibu wa Movenpick Royal Palm SACCOS, Abiel Mkongwa ambaye alikuwa Mwenyekiti wa mafunzo hayo akizungumza.
Na Dotto Mwaibale, Dar es Salaam.
TUME ya Maendeleo  ya Ushirika Tanzania (TCDC) imetoa angalizo hadi ifikapo Oktoba 10 mwaka huu mtu au chama chochote cha ushirika kinacho jishughulisha na masuala ya huduma ndogo za fedha ambacho kitakuwa hakina leseni hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
Hayo yamebainishwa  na Mrajis Msaidizi anayesimamia Vyama vya Ushirika wa Kifedha kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC), Josephat Kisamalala wakati akizungumza katika mafunzo ya siku mbili kwa viongozi na watendaji wa Vyama vya Akiba na Kukopa (SACCOS) Mkoa wa Dar es Salaam.
" Ifikapo muda huo mtu yeyote au chama cha ushirika kitakachobainika kujishughulisha na hutoaji wa huduma za fedha bila leseni adhabu yake ni faini ya kuanzia milioni 10 hadi 50 au kifungo cha miaka miwili hadi mitano au vyote kwa pamoja kama sheria ya huduma ndogo ya fedha ya 2018 inavyoelekeza" alisema Kisamalala.
Alisema Tume hiyo inatoa mafunzo hayo yenye lengo la kuwajengea uwezo viongozi wa vyama hivyo ili waweze kuijua sheria hiyo na kuwa maombi ya leseni hizo yatatolewa kwa njia ya mtandao na ndani ya siku 60 muombaji atakuwa amepata leseni yake baada ya kukidhi vigezo.
Alisema kuwa mafunzo hayo tayari yametolewa katika mikoa ya Singida, Mbeya, Mwanza, Kagera, Ruvuma na Songwe ambapo yataendelea Tanga, Kilimanjaro, Iringa na Morogoro na kuwa wameyaweka katika kanda ili kurahisisha utowaji wake.
Naibu Mrajis wa Vyama vya Ushirika, Collins Nyakunga alisema sheria hiyo iliyopitishwa na Bunge na kuipa mamlaka  Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kusimamia SACCOS zote hapa nchini itaondoa changamoto zilizokuwepo kama vile utoaji wa riba kubwa kwa wakopaji.
Kwa upande wake Katibu Tawala Msaidizi sehemu ya uchumi na uzalishaji Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Elizabeth Mshote alisema sheria hiyo itaondoa malalamiko kutoka kwa wananchi waliokuwa wanavilalamikia vyama hivyo.

No comments:

Post a Comment