Kamati ya  Kudumuya Bunge ya Katiba na Sheria iliyoshirikisha viongozi wa juu wa Wizara ya Katiba na Sheria na Mahakama wamefanya ziara ya  ukaguzi wa majengo  yanayojengwa na Mahakama ya Tanzania katikaWilaya za Kondoa  mkoani Dodoma, Babati mkoani Manyara, na Longido mkoaniArusha ambapo kamati imeonesha kuridhishwa na kazi nzuri inayofanywa naMahakamaya Tanzania katika maeneo yaliyotembelewa.
Akizungumza   na  Kitengo  cha  Habari  na Mawasiliano Serikalini wakati wa ziara hiyo Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Tabora  mjini Mhe. Emmanuel Mwakasaka amempongeza Rais wa  Jamhuri  ya Muungano  wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa  uongozi wake mahiri ambao ndiyo chachu ya ujenzi wa Mahakama nyingi nchini kwasasa.
 Kondoa, Manyara, Longido ambazo zimekamilika ni mfano wa mahakama nyingi zilizojengwa na zinazoendeleakujengwa kwa kasi hapa Tanzania.
“Kwanza tumpongezeMhe.RaisDkt. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa uongozi wake madhubuti katika kuhakikisha kwamba haki inapatikana kwaharaka na kwawakati. Kasi ya ujenzi wa majengo haya ya Mahakamani wa kupigiwa mfano, niwapongeze sana watendaji wote wa Mahakama”, amesema Mwakasaka.
Kwaupande wake Waziri wa katiba na sheria ,Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga pamoja na kupongeza uzuri na ubora wa majengo ya Mahakama zote walizotembelea, alionesha kufurahishwa na uimara wa samani zilizowekwa katika Jengo la Mahakama yaL ongido hivyo, ametoa rai kwa uongozi wa Mahakama kuzingatia utunzaji wa samani na majengo ya mahakama zote nchini hususani zilizojengwa na zinazoendelea kujengwa.
“Hizi samani zilizowekwa katika Mahakama hii ni za kiwango cha juu na zimetengenezwa kwa mbao zilizozalishwa hapa nchini na waliotengeneza ni mafundi wazawa, hongereni sana watendaji wote mliohusika kutekeleza jambo hili,” amesema Balozi Mahiga.
Ziara ya  Kamati  ya Kudumu ya Bunge katika  mikoa ya Dodoma, Manyara  na Arusha imeendelea  leo Machi 15,2020 ,kwa kukagua ujenzi wa Jengo la ghorofa nne la Mahakama Kuu ya Kanda ya Arusha ambalo imeelezwa  pia litatumika kama kituo jumuishi cha  utoaji haki.
Aidha, imethibitika kwamba majengo kama la Mahakama Kuu ya Kanda ya Arushayatajengwa katika mikoa  ya Dodoma, Mwanza, Dar es Salaam, Morogoro na Arusha yenyewe.

Ukaguzi huo pia umefanyika katika majengo yaMahakama Kuu ya  jiji la Arusha na wiki kesho  utaedelea katikaMkoa wa Morogoro.





Waziri  wa Katiba na SheriaMhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (kulia) akizungumza jambo na Kaimu Mwenyekiti wa Kamati yaKudumu ya Bunge yaKatiba na SheriaMhe. Emmanuel Mwakasaka wakati wa ziara ya Kamati hiyo ya kukagua ujenzi wa jengo la Mahakama Kuu Kanda yaArusha.
Baadhi ya Mafundi wakiendelea na ujenzi waj engo la ghorofa nne la Mahakama Kuu Kanda ya Arusha ambalo pia litatumika kama kituo jumuishi cha utoaji haki.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na SheriaProf. Sifuni Mchome (katikati) pamoja na baadhi yaWajumbe wa Kamati yaKudumuya Bunge ya Katiba na Sheria wakivaa vifaa vya kujilinda  muda mfupi kabla ya kuanza ukaguzi wa ujenzi wa jengo la Mahakama Kuu Kanda yaArusha.

Ujenzi  wajengo la ghorofa nne la Mahakama Kuu Kanda ya Arusha ukiendelea kwa kasi

 Jengo la Mahakama ya Wilaya ya Longido, jijiniArusha.

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria katika picha ya pamoja mbele ya jengo la MahakamayaWilaya yaLongido, mkoaniArusha.

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria wakipokea maelezo kuhusu kukamilika kwa ujenzi wajengo la Mahakama ya HakimuMkazi-Manyara.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome akizungumza jambo na baadhi ya wananchi wakatiwaziara yaKamati ya  Kudumu ya Bunge ya Katiba naSheria ya ukaguzi wa Makama ya Hakimu Mkazi-Manyara.
Waziri wa Katiba na Sheria Balozi Dkt. Augustine Mahiga akizungumza jambo na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Amon Mpanju wakati waziara ya Kamati ya Kudumu ya  Bunge ya Katibana Sheria mkoani Manyara. Kuliani  Prof. Sifuni Mchome, Katibu MkuuWizara ya Katiba naSheria.

Katibu  Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome (kulia) pamoja na baadhi yaWajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria wakati wa ukaguzi wa ujenzi wajengo la Mahakama ya HakimuMkazi-Manyara.Kuliani Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi wa Majengo cha Mahakamaya Tanzania Mhandisi Khamadu Kitunzi.

Mheshimiwa  BaloziDkt. Augustine Mahiga akikagua samani katika jengo la Mahakama yaWilaya yaLongido jijiniArusha.
Baadhi ya Wajumbe  wa KamatiyaKudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria wa kikagua samani katika moja ya chumba cha Mahakama yaWilaya ya Longido jijini Arusha.
Share To:

Post A Comment: