Mlezi wa CCM Mkoa wa Morogoro ambae pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Bara Rodrick Mpogolo leo Jumamosi 08 Februari 2020 ameweka jiwe la msingi Jengo la kisasa CCM wilaya ya Gairo na uwanja wa Mpira wa kisasa unaomilikiwa na CCM wilayani hapo.

Jengo la ofisi ya Wilaya  hadi kukamilika kwake litagharimu jumla ya  T. Sh 287,533,750 mbapo hadi hatua iliyofikia  zimetumika  Shillingi 92,685,780/=  nguvu za wanachama, viongozi na wadau mbali mbali wenye mapenzi mema na CCM wakati uwanja wa mpira katika hatua za awali umegharimu zaidi ya T.Sh 156,000,000/= zilizotolewa na Mbunge wa Jimbo la Gairo Ahmedi Shabiby

Hatua hiyo ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 43 ya Kuzaliwa kwa CCM ambapo Mkoa wa Morogoro zimeadhimishwa wilayani Gairo  na kuhudhuriwa na viongozi, wanachama na wananchi kutoka Wilaya 8 za kichama za mkoa huo.

Akizungumza Katika Maadhimisho Hayo yaliyofanyika Viwanja vya Shule Ya Msingi ya Gairo A Naibu Katibu Mkuu Mpogolo amekemea Vikali Tabia ya Viongozi wa Chama hicho Kuacha kubeba wagombea mfukoni kipindi cha uchaguzi
"Kwenye Majimbo naona baadhi ya wana CCM wameanza kupasha niwaambieni tu Muda bado. Kuna Tabia ya baadhi ya Viongozi Kubeba wagombea kwa Maslahi yao Nawakumbusha Kanuni za Uchaguzi ni Mwiko Nadhani ujumbe umefika"
Share To:

msumbanews

Post A Comment: