Washiriki wakiwa jukwaani 


NA ANDREW CHALE, BUSEGA.
VAZI  la Kabila la Wamasai lililobuniwa kiasili limeweza  kuwa kivutio kikubwa katika shindano la Urembo wa Asili kwenye tamasha la kukuza na kuendeleza Utalii Wilaya ya  Busega la 'LAMADI UTALII FESTIVAL'.

Katika tukio hilo  Wanawake mbalimbali wameweza kuonesha namna unavyoendeleza tamaduni kwa kuendelea kutumia vitu vya asili ikiwemo urembo na mavazi.

Washiriki hao wameweza kuonesha namna makabila yao wanavyodumisha asili pamoja na tamaduni zenye kujenga na kuendeleza jamii.

Katika tukio la urembo wa asili, binti kutoka kabila la Masai, Selina Tate Molell alikuwa gumzo kutokana na ubunifu wa vazi lake sambamba na urembo wa asili ikiwemo nakishi za shanga na michoro kwenye mwili ambayo inamaana mbalimbali kwenye koo zao.

Mshiriki huyo kupitia vazi lake pja alizua gumzo namna ya asili ya koo  na kabila lao hilo  wakati wa kuelezea uelewa wa asili wake.

Aidha, washiriki wengine wakiwemo kabila la Wakurya, Wajita, Wasukuma na Wasanzu  walielezea namna ya mila na tamaduni zao kwa ujumla toka asili za koo zao.

Nae Mkuu wa Wilaya ya Busega ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya tamasha hilo, Bi. Tano Mwera alisema wataendelea kuhakikisha wanadumisha mila na tamaduni za makabila yote sambamba na kupinga ukatili wa kijinsia wanaofanyiwa wanawake.

Tamasha hilo ni la msimu wa kwanza ambapo lilianza Desemba 29 na kutarajiwa kufikia tamati Leo Januari Mosi 2020.

Mwisho
Share To:

Francis Godwin Mzee wa matukiodaima

Post A Comment: