Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Mafinga Charles Makoga akifunga kikao cha kupitisha bajeti ya Halmashauri
Madiwani wa Halmashauri ya Mji Mafinga wakipitia makisio ya bajeti kwenye kikao
Baraza la madiwani la Halmashauri ya Mji Mafinga mkoani Iringa limeidhinisha makisio ya bajeti ya shilingi milioni 24.9 kwa mwaka 2020/2021 kwa ajili ya matumizi ya mishahara miradi mbali mbali ya kimaendeleo ikiwemo ya ujenzi wa barabara za kiwango cha lami katika mitaa ya mji wa Mafinga .
Kaimu afisa mipango wa Halmashauri ya Mji Mafinga Mashaka Mkongwa akisoma makisio ya bajeti hiyo kwenye kikao cha kuidhinisha bajeti cha baraza la madiwani ya Mji Mafinga jana alisema kuwa kati ya fedha hizo mapato ya ndani ya shilingi 4,613,800.100 makisia ya mapato ya ndani ni zaidi ya shilingi 638,721,000 ambayo ni sawa na asilimia 16.00 ukilinganisha na makisio ya mwaka 2019/2020 ya shilingi 3,975,079.100.
Pia kwenye mapato hayo kiasi cha shilingi 798,493,500 ni mapato ya vyanzo fungiwa katika idara ya afya na elimu sekondari hivyo kufanya mapato halisia kuwa ni shilingi 3,815,315,306.600.
Hata hivyo alisema kwa mwaka 2020/2021 jumla ya shilingi 18,428,460.00 zimeombwa kwa ajili ya matumizi ya kwaida na mishahara ,kati ya fedha hizo kiasi cha shilingi 14,757,136,020.00 ni kwa ajili ya mishahara na shilingi 3671,602,440.00 ni kwa ajili ya matumizi mengineyo na chanzo cha fedha hizo ni makusanyo ya mapato ya ndani na serikali kuu .
Aidha alisema katika mpango wa bajeti ya maendeleo ya mwaka 2020/2021 Halmashauri ya Mji Mafinga inatarajia kukusanya na kutumia kiasi cha shilingi 6,537,959,035.16 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo fedha zitakazotokana na vyanzo mbali mbali na kati ya fedha hizo shilingi 4,431,302,708.16 ni toka ruzuku ya serikali kuu ,wahisani ni shilingi 580,533,687 na Halmashauri itachangia kiasi cha shilingi 1,526,122,640,00 sawa na asilimia 40 ya mapato halisi ya ndani .
Alisema kuwa kwa mwaka wa fedha 2019/2020 Halmashauri hiyo iliidhinishiwa kukusanya na kutumia kiasi cha shilingi 23,752,127 ikiwa shilingi 12,654,625,953.00 ni za mishahara ,kiasi cha shilingi 1,060,615,016.00 ni matumizi ya kawaida na kiasi cha shilingi 6,246,137,825.66 kwa ajili ya miradi ya maendeleo kutoka serikali kuu na wafadhili .
Pia kati ya fedha hizo Halmashauri iliidhinishiwa kukusanya na kutumia kiasi cha shilingi 3,975,079,100.00 kutoka makusanyo ya mapato ya ndani ambapo kiasi cha shilingi 2,022,395,460 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida sawa na asilimia 60 na kiasi cha shilingi 1,348,240 ni kwa ajili ya miradi ya kawaida sawa na asilimia 40 na kiasi cha shilingi 604,420,000.00 ni mapato fungiwa .
Hata hivyo alisema hadi kufikia Desemba 31 2019 jumla ya shilingi 8,273 ,101,339.83 zimetumika sawa na asilimia 92.68 ya fedha zilizopokelewa kwa ajili ya matumizi ya wakawaida ,mishahara na miradi ya maendeleo kuwa kati ya fedha zilizotumika kiasi cha shilingi 5,759,191,620 ni kwa ajili ya mishahara ,shilingi 431,411,732.43 ni matumizi mengineyo na shilingi 818,155,448.49 ni miradi ya maendeleo .
Pia alisema wadau na wananchi walichangia kiasi cha shilingi 56,870,654.88 katika miradi ya maendeleo fedha ambazo ziliweza kutekeleza miradi mbali mbali na wananchi wenyewe .
Kupitia bajeti hiyo wameweza kuongeza ufaulu wa wanafunzi wa darasa la saba umefikia asilimia 93 ambapo wamekuwa wa pili kimkoa na 17 kitaifa kwa mwaka 2019 ,ujenzi wa jengo la utawala umekamilika na kukamilika kwa jengo hilo kutaboresha utoaji wa huduma za kiutawala kwa wananchi .
Mkongwa alisema kuwa kumekuwepo na mafanikio makubwa katika utekelezaji wa bajeti kwa mwaka 2019/2020 kwa kipindi cha nusu mwaka kwa maana ya Julai -Desemba 2019.
Akitolea mfano wa mafanikio hayo alisema ni pamoja na upatikanaji wa dawa .vifaa tiba na vitendanishi umeimarika na kufikia asilimia 100 kwenye zahanati na vituo vya afya na asilimia 97 kwa Hospitali .
Pia Halmashauri imeendelea kufanya vizuri katika kusimamia ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa kufikia asilimia 56 katika kipindi cha nusu mwaka , hali ya usafi wa mazingira katika Mji imeboreshwa na Halmashauri imekuwa ya mshindi wa tatu kitaifa katika mashindano ya usafi wa mazingira .
Aidha ujenzi wa shule mpya ya sekondari ya kata ya Upendo umekamilika na imepokea wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka2020 na imepata usajili tayari ,ujenzi wa soko la kuuzia mboga na matunda lililopo uwanja wa Mashujaa limepauliwa na linatumika na kiasi cha shilingi 161,093,599.94 zimetolewa na Halmashauri kwa ajili ya kuanza mchakato wa kukopesha vikundi vya vijana ,wanawake na walemavu sawa na asilimia 47.7 ya lengo la kukopesha kiasi cha shilingi 337,065,910
Alisema changamoto kubwa iliyojitokeza katika utekelezaji wa bajeti hiyo ilikuwa ni upungufu wa watumishi katika idara mbali mbali ,upungufu wa vitendea kazi kama magari ,vifaa vya tiba ,samani kuhusu magari alisema magari mengi yaliyopo ni chakavu na hayatoshelezi idara zote .
Akizungumza baada ya kupitisha makisio hayo ya bajeti,mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Mafinga Charles Makoga alisema kuwa fedha hizo zilizopitishwa zitaendelea kuleta kasi kubwa ya maendeleo katika Halmashauri hiyo .
Huku akiwataka watumishi wa umma katika halmashauri hiyo kwenda kufanya kazi kuwatumikia wananchi ili kufanikisha malengo ya Halmashauri hiyo badala ya kwenda kufanya kazi ya siasa na kutaka kuwakwamisha wanasiasa ili wasichaguliwe kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika octoba mwaka huu .
Post A Comment: