Madaktari na wauguzi wa kituo cha afya Malangali Katika Halmashauri ya Mufindi wakiwa wamefanikiwa kufanya upasuaji salama wa kwanza 


 Halmashauri ya wilaya ya Mufindi mkoani Iringa inaendelea kutekeleza ilani ya CCM  leo kituo cha afya Malangali kimefanikiwa kufanya upasuaji wa kwanza salama  wa kihistoria .

Akizungumza baada ya zoezi hilo kubwa na la mafanikio kwa sekta ya afya mkurugenzi wa Halmashauri ya Mufindi Netho Ndilito alisema kuwa kituo hicho ni miongoni mwa vituo 352 vya Afya Tanzani vilivyoboreshwa na serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais Dkt.John  Msgufuli .

Hivyo alisema jitihada kubwa zinazofanywa na serikali kwa Halmashauru ya Mufindi wanapongeza sana hasa baada ya kilio chao kupatiwa majibu .

" kwa mara ya kwanza kituo cha afya Malangali  kimeanza kutoa huduma ya uasuaji baada ya Rais Dkt.John  Magufuli  kutupatia vifaa vya kisasa vyenye thamani ya Tsh milioni  204"

 Alisema Januari 21 mwaka huu majira ya  saa tano usiku  timu ya wataalamu madaktari na wauguzi walifanya upasuaji wa kwanza na wa  kihistoria  wa mama mjamzito katika kituo  hicho cha Afya cha Malangali.

 Hivyo alisema ni furaha kubwa  kwa serikali ya wilaya ya Mufindi chini ya mkuu wa wilaya Jamhuri Wiliam ,madiwani wote kupitia mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Festo Mgina kwa utekelezaji wa miradi ya kimaendeleo kwa pamoja na kupata matokeo mazuri kupitia kituo hicho kwa kupata mwanafamilia mpya mtoto wa kike aliyepatikana kwa upasuaji salama .


"Shukrani za pekee kwa Serikali yetu ya awamu ya tano chini ya  Rais wetu mpendwa Dkt.John pombe Magufuli  kwa kuendelea kugusa maisha na nafsi  za Watanzania zawadi kubwa kwake ni kuendelea kumuombea zaidi "

Alisema Halmashauri hiyo na wananchi wake wameendelea kunufaika na utendaji kazi mzuri .

" Tukishindwa kumshukuru kwa vinywa vyetu wenyewe kwa Rais Dkt John   Magufuli anayeokoa maisha yetu basi tujiandae kuhukumiwa ahela, mimi na Wananchi wa Halmashauri ya MUFINDI tunakushukuru sana sana mheshimiwa Rais  kwa kuendelea kujali, kutambua na kuthamini maisha yetu lakini pia kutuletea Maendeleo makubwa na ya kihistoria katika Halmashauri yetu ya Mufindi Mungu akubariki sana"alisema Ndilito


Share To:

Francis Godwin Mzee wa matukiodaima

Post A Comment: