Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha  amefungua Mkutano wa Wa Jumuiya ya Watafiti wa rasilimali vitu ya Afrika na kuwataka watafiti  hao kufanya tafiti zinazotatua changamoto mbalimbali katika jamii pamoja na kusaidia katika kujibu mahitaji ya viwanda ili kuwezesha kukua kwa uchumi wa viwanda nchini Tanzania na Afrika kwa ujumla.

Akizungumza katika Mkutano wa Jumuiya ya Watafiti katika rasilimali vitu ya Afrika uliofanyika katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela ,Nasha amesema kuwa tafiti zinapaswa kulenga mahitaji ya jamii na kusaidia jamii katika matatizo mbalimbali hivyo amewataka watafiti kuangalia mahitaji ya jamii zaidi kuliko kufanya tafiti ambazo haziwafikii wananchi moja kwa moja kwa maana ya kukidhi mahitaji yao na mahitaji ya viwanda.

Aidha Ole Nasha amewataka Watafiti hao kuwa na agenda za utafiti kutoka barani Afrika kulingana na mahitaji kuliko kusubiri kuamuliwa agenda za utafiti na mataifa mengine bila kujali vipaumbele vya utafiti katika bara la Afrika.

Raisi wa Jumuiya ya Watafiti wa rasilimali vitu  ya Afrika ,Profesa Hulda Swai amesema kuwa mkutano huo umejumuisha watafiti kutoka nchi 38 za Afrika na nje ya bara hilo lengo ikiwa ni kubadilishana uzoefu juu ya tafiti na kutumia matokeo ya utafiti kusaidia jamii hivyo Mkutano huo utafungua milango ya ushirikiano kati ya watafiti wa bara la Afrika na nje ya bara hilo.

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Sayansi cha  Nelson Mandela ,Profesa Emmanuel Luoga amesema kuwa Afrika ina rasilimali nyingi sana lakini hakuna wataalamu wa kutosha kubadili rasilimali hizo kuwa huduma au bidhaa na pia kuchochea maendeleo ya watu pamoja na viwanda.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: