Monday, 2 December 2019

MRADI WA REGROW KUBORESHA MIUNDO MBINU HIFADHI YA RUAHA

Katibu mkuu wizara ya maliasili na utalii Prof Adolf Mkenda wa pili kushoto akiwa na kamishinda mwandamizi wa hifadhi za Taifa (TANAPA) kanda ya kusini Dkt Christopher Timbuka kushoto na watumishi wa hifadhi ya Ruaha wakikagua eneo la kujenga daraja la kuunganisha mkoa wa Mbeya hadi Dodoma kupita ndani ya hifadhi hiyo jana Picha na habari na Francis Godwin
...................................................
 Katibu   mkuu  wizara ya maliasilia  na utalii Prof Adolf Mkenda amesema   wizara  yake  imejipanga kupitia mradi wa kuendeleza Utalii Ukanda wa Kusini mwa Tanzania(REGROW) kuboresha  miundo mbinu ya  hifadhi ya Taifa ya  Ruaha  mkoani  Iringa  ili  kuweza  kuvutia  idadi kubwa ya  watalii  zaidi .

Akizungumza  jana  baada ya  kuzindua   vitendea  kazi  vya  mradi wa REGROW  katika  hifadhi ya Taifa ya  Ruaha  katibu  mkuu  huyo  alisema  kuwa  wizara   hiyo  imeelekeza  nguvu  zake  kutangaza na  kuboresha  miundo mbinu  katika  hifadhi ya Ruaha   ili  kuiwezesha   hifadhi  hiyo  na hifadhi nyingine kuendelea  kujiendesha  kwa  faida   na  kutoa gawio lake  serikalini .

Kwani  alisema changamoto ya  miundo mbinu katika  maeneo ya  hifadhi  mbali mbali  hapa nchini  imekuwa kikwazo kikubwa kwa  watalii kufika  kutembelea  hifadhi nchini  na kama  miundo mbinu itaboreshwa  watalii  zaidi  wanaweza  kufika  kwa urahisi  zaidi .

Alisema  changamoto kubwa ya  hifadhi ya Ruaha  ni pamoja na ubovu wa miundom mbinu na  kuwa kupitia mradi  wa REGROW   wizara  imejipanga  kuanza  kuboresha  miundo mbinu  hiyo na  kutangaza  hifadhi  ya Ruaha  ili  kuwezesha   kuongeza kasi ya  watalii  kufika .

Prof Mkenda  alisema    changamoto  ya  utalii ina  vitu viwili  vikubwa kwanza kufungua  miundo mbinu ndani ya  hifadhi yenyewe  na namna ya  kufikia  ndani ya  hifadhi  hivyo mradi huo  unasaidia mambo makubwa mawili  kutangaza na kuboresha  miundo mbinu  yake .

Alisema  ndani ya  hifadhi ya  Ruaha  wanategemea  kupitia mradi   huo wa REGROW  kufungua  barabara  ya kuunganisha  mkoa wa Mbeya na Dodoma   kwa  kujenga  daraja  kubwa katika eneo la Othuman  ambalo  kuna mzungu   alipata  kujenga  daraja  kabla ya  hifadhi  hiyo  kutangazwa  rasmi kuwa  kujengwa kwa daraja   eneo hilo kutawezesha   kuunganisha  hifadhi  hiyo  na  watalii  wakaweza kuingia kutokea  Dodoma na  kutokea Mbeya kwenda  hifadhi nyingine kama Katavi  na Kitulo  .

Hata  hivyo  alisema  wakati  wizara  inaendelea   kufanya  jitihada za  kutangaza  utalii na kuboresha  miundo mbinu mbali mbali kwenye hifadhi  nchini  bado  itatoa wito kwa wadu wa utalii  nchini  kuunga mkono jitihada za  kutangaza utalii  kwa kutenga  gharama  zao  wenyewe  badala ya  kusubiri  kuwezeshwa na wizara  ya  maliasi  na utalii kwa kila jambo  wanalotaka kufanya .

Kwani  alisema  wapo  baadhi ya  wadau  wa ndani ya  nchi na nje ya nchi  ambao  wameendelea  kutangaza  utalii nchini kwa kutumia gharama  zao  wenyewe  .

Japo  alisema   wizara  itaendelea  kuwatumia  watu  wa makundi mbali mbali  watu maarufu kwa ajili ya kutangaza  utalii  nchini japo watafanya  hivyo kwa kushirikisha idara  mbali mbali  zinazohusiana na makundi hayo  ili  kuweka  vigezo  vya  kuwapata  wale  watakaofanya kazi  ya kutangaza  utalii  na mwisho wa siku kuja na matokeo ya kazi hiyo .

Prof Mkenda alisema  kuwa  wakati wanaendelea na uboreshaji wa  miundi  mbinu  katika  hifadhi nchini  bado  wizara  inaangalia  jinsi ya kuanzisha   utalii  wa  meli na fukwe ili  kuvutia  watalii  zaidi  nchini  kwani  wapo  baadhi ya  watalii  ambao  wanatamani  kuja  kutalii katika hifadhi  za fukwe na utalii  wa meli na  kuwa  jitihada zitakazofanyika ni  kujenga  magati kwa  ajili ya utalii  wa meli na kuboresha maeneo ya  fukwe .


Kamishna mwandamizi wa uhifadhi wa  hifadhi  za  Taifa  (TANAPA ) kanda ya  kusini  Dk Christopher Timbuka  alisema  kuwa  ujio wa mradi wa REGROW  umetokana na changamoto ambazo hifadhi  za kusini  zilikuwa  zikikabiliwa  nazo .

Kuwa  changamoto hizo ni miundo mbinu  kuwa mibovu na  watalii kushindwa kufika katika  hifadhi   hivyo mradi huo  utawezesha kufungua  utalii   nyanda  za  kusini .

Hivyo  alisema  ujio wa mradi huo  ambao unaanza kazi  utasaidia  kuongeza idadi ya watalii na kuongeza idadi ya  vitanda  kutoka  vitanda  400  vilivyopo na kuongezeka zaidi ili  watalii  kuweza kupata maeneo ya  kufikia .

Alisema  kupitia  mradi huo  ulinzi  ulinzi  didhi ya ujangili  kwenye hifadhi  utapungua zaidi  kutokana na mradi  huo  kuwezesha  vitendea kazi vya  kisasa kwa ajili ya kuimarisha  ulinzi .

Mratibu  wa  mradi wa REGROW Saanya Aenea  alisema  kuwa vifaa  mbali mbali  vimezinduliwa kwa  ajili ya mradi  huo na kuwa  changamoto  kwa  asilimia 100  zitakwenda  kumalizika  .

Pia  alisema  kwa  kupitia mradi huo wananchi  watajengewa  miradi  ya  kiuchumi kama  ya ufugaji samaki ,ufugaji nyuki na mingine  ili  kuwawezesha  kiuchumi  na  wasiwe chanzo cha  kujihusisha na ujangili .

Vifaa vya Regrow 

No comments:

Post a comment