Baba Askofu Mstaafu wa Kanisa la Evangelist Assemblies of God Tanzania (EAGT) Dkt. Asumwisye Mwaisabila ambaye atakuwa mgeni rasmi katika kilele cha kongamano hilo. 
Bishop Flaston Ndabila (kulia) na Mke wake Janeth Ndabila wa Kanisa la ABC Tabata waandaaji wa Kongamano na Tamasha la Uimbaji  wakiwa katika picha ya pamoja. Tamasha hilo litakwenda sanjari na kuwapongeza wanandoa hao kwa kutimiza miaka 25 ya ndoa, miaka 25 ya huduma na miaka 50 ya kuzaliwa. 
 Bishop Robson Simkoko kutoka Malawi.
 Bishop Mark Mugekenyi Kairuki (Kenya)
 Bishop Musa Ngobese (Afrika Kusini).
Pastor Fred Msungu.
 Pastor Hererimana Tharcise (Burundi) 
Apostle Moses Silwamba (Zambia) 
Na Dotto Mwaibale.
MAASKOFU 30 na wachungaji 80 kupamba Kongamano na Tamasha la jimbo za Injili jijini Dar es Salaam.
Kongamano na Tamasha hilo limeandaliwa na Kanisa la ABC lililopo Barabara ya Mandela Tabata na kuwa maandalizi yake yamekwisha kamilika.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Mratibu wa Kongamano hilo, Askofu Flaston Ndabila alisema maandalizi yote yamekamilika na kuwa siku ya hitimisho ambayo itakuwa ni Desemba 9  mgeni rasmi atakuwa ni Baba Askofu mstaafu wa Kanisa la Evangelist Assemblies of God Tanzania (EAGT) Dkt. Asumwisye Mwaisabila 
mwenye kalama kubwa ya uneneji.
"Makongamano hayo ya vijana, wanandoa na sherehe tunatarajia kuwa na washiriki zaidi ya 200, maaskofu 30 na wachungaji 80 kutoka ndani na nje ya nchi" alisema Ndabila.
Alisema kongamano la vijana litakuwa la siku moja ya Desema 6 na litafanyika kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi saa 9:00 jioni na tamasha la uimbaji walengwa ni vijana kutoka vyuo vikuu na makanisa mbalimbali.
Askofu Ndabila aliongeza kuwa Desemba 7 kutakuwa na kongamano maalumu la ndoa na familia ambalo litahusisha maaskofu na wachungaji hao.
Aliwataja baadhi ya watumishi hao wa mungu watakaohudhuria kongamano hilo kuwa ni Bishop Robson Simkoko kutoka Malawi, Mchungaji Moses Silwamba (Zambia), Pastor Hererimana Tharcise (Burundi)  Pastor Fred Msungu na muimbaji wa nyimbo za injili kutoka jijini Arusha, Eliya Mwantondo.
Wengine ni Bishop Mark Mugekenyi Kairuki (Kenya) na Bishop Musa Ngobese (Afrika Kusini).
Kwa mawalisiano zaidi kuhusu kongamano hilo unaweza kupiga simu namba 0754762301 na 0715684590.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: