Katibu tawala msaidizi wa Serikali za mitaa mkoani Ruvuma Joel Mbewa akitangaza matokeo ya darasa la saba mkoani humo ambapo kimkoa mwaka huu ufaulu umepanda.
.


 Baadhi ya wajumbe wakifuatilia matokeo ya mitihani ya darasa la saba wakati yakitanganzwa
..........................................................

  KATIBU tawala msaidizi wa Serikali za mitaa mkoani Ruvuma Joel Mbewa amewataka wakurugenzi na maafisa elimu wa Halmashauri za mkoani humo kufanya utaratibu wa kuwapongeza walimu wa Halmashauri hizo kutokana na kazi za kuongeza ufaulu kwa wanafunzi MWANDISHI AMON MTEGA ANARIPOTI KUTOKA RUVUMA .

 Wito huo aliutoa  wakati akitangaza matokeo ya darasa la saba ya mkoani humo ambapo katika msimu wa mwaka huu wa 2019 ufaulu kimkoa umeongezeka tofauti na kipindi kilichopita cha mwaka 2018.

 Mbewa akitangaza matokeo hayo mbele ya wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa Halmashauri za mkoani humo amesema kuwa ufaulu huo umeongezeka kutokana na walimu kujituma kufundisha pamoja na kuongeza maarifa hivyo ni vema Halmashauri zikatafuta namna ya kuwapongeza ili kuwatia moyo katika utendaji kazi.

 Aidha alizitaja Halmashauri zilizoongoza katika ufaulu kimkoa kuwa ni Tunduru ambaye kitaifa imeshika nafasi ya 28 ,na Halmashauri ya Manispaa ya Songea imekuwa ya pili kimkoa na kitaifa imekuwa nafasi ya 32.

  Hata hivyo amesema kuwa bado kumekuwepo na utoro wa wanafunzi mashuleni hivyo aliwataka wakurugenzi kwa kushirikiana na walimu pamoja na wazazi kwenda kuvikomesha vitendo hivyo  na kuhakikisha wanafunzi wote wanahitimu shule .

“Serikali ya awamu ya tano  imejipanga kikamilifu katika kuendelea kuboresha sekta ya elimu hivyo haya mafanikio makubwa yaliyopatikana kwenye ufaulu huu ni moja ya matokeo ya mipango mizuri ya serikali na waliyofaulu wote wataenda kujiunga na Sekondari kwa asilimia 100”amesema Joel Mbewa.

  Pia amewataka wakurugenzi ambao baadhi ya shule zao majengo yake yameezuliwa kwa mvua zinazoendelea kunyesha, majengo hayo yaweze kufanyiwa ukarabati ili wanafunzi waweze kuendelea na masomo .

                     

Share To:

Francis Godwin Mzee wa matukiodaima

Post A Comment: