NA HERI SHAABAN

SERIKALI inatarajia kubomoa nyumba zaidi ya 20 Kata ya Vingunguti kwa ajili ya upanuzi wa Machinjio ya kisasa.

Hayo yalisemwa na MEYA wa Halmashauri ya Ilala Omary Kumbilamoto  Vingunguti Manispaa Leo, katika mkutano wa hadhara wakati wa kuwatambulisha Wenyeviti wa Serikali za Mitaa  sita waliochaguliwa kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM.

" Ujenzi wa Machinjio ya kisasa ya Serikali yaliopo  Vingunguti umefikia asilimia 64 kwa sasa ujenzi wake unatarajia kumalizika hivi karibuni katika ujenzi huo nyumba  zaidi ya 20 zitavunjwa Mtaa  wa Butihama kwa ajili ya kupata eneo la kushushia ng' ombe " alisema Kumbilamoto.

Meya Kumbilamoto amesema hivi karibuni Wataalam wa Halmashauri watapita katika mtaa huo kwa ajili ya kufanyia tathimini ili waweze kulipwa.


Ujenzi wa Machinjio ya Vingunguti ulianza hivi karibuni  ni moja ya mradi wa mkakati wa Serikali ya awamu ya tano  ya Tanzania ya uchumi wa Viwanda .

Awali Rais John Magufuli alitembelea eneo LA Machinjio hayo na kuagiza Mkandarasi wa ujenzi huo akabidhi Desemba mwaka huu,Desemba 03 Mwaka huu Waziri Mkuu alifanya ziara katika Machinjio hayo kuangalia ujenzi wake unavyoendelea.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa Miembeni Hamis Chogelo alisema atashirikiana na Jeshi la polisi ili kuakikisha usalama unakuwepo wa kutosha kutokana na sasa hivi eneo hilo usalama mdogo kutokana na vibaka..

Chogelo alisema atashitikiana na Serikali iliyomuweka madarakani pamoja na CHAMA cha mapinduzi katika kutatua changamoto za wananchi.

Aliomba ushirikiano wa Wananchi wake wa mtaa huo ili kuleta Maendeleo katika kuibua miradi ya Maendeleo na kuisimamia.

Mwisho
Share To:

msumbanews

Post A Comment: