Mwajuma Mfaume(23) mkazi wa mtaa wa Kibulang’oma kata ya Lizaboni Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma akiendelea kutoweka 

 Mateso anayopata ni Mungu tu anajua ni binti Mwajuma Mfaume(23) mkazi wa mtaa wa Kibulang’oma kata ya Lizaboni Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma anaiomba Serikali pamoja na wadau mbalimbali waweze kumsaidia kupatiwa matibu ya maradhi ya kuugua mgongo ambao unakidonda kikubwa yapata miaka miwili sasa.Mwandishi wetu Amon Mtega anaripoti toka Songea

 Akizungumza na MTANDAO huu  amesema kuwa maradhi hayo yalimkuta mwezi wa tisa mwaka 2017 majira ya saa nane usiku akiwa amelala chumbani kwake.

   Mwajuma amesema kuwa akiwa amelala alijisikia mgongo unawaka moto na alipo amka na kuugusa alikuta ngozi yote imeshanyofoka inabembea huku akikutwa na maumivu makali.

 Amesema kuwa baada ya tukio hilo mama yake mzazi Fatuma Bashiru [40]alimpeleka Hospital ya misheni Peramiho ambako alitibiwa bila kupata mafanikio ya ugonjwa huo  na hatimaye wakamua kulejea  Nyumbani kwao.

 Ameeleza kuwa walipokuwa nyumbani wakashauriwa na majirani zao waende Hospitali ya rufaa ya mkoani Ruvuma na walipofika Hospitalini hapo walianza tena matibabu ambapo kidonda kilikuwa kikisafishwa kwa Sh.45,000/=na mwisho wa siku walishindwa kumudu garama hizo kutokana na kidonda hicho kutokuonyesha dalili za kupona.

“Nina maumivu makali sana ninalala kifudifudi muda wote mama yangu anapata taabu sana namna ya kunihudumia sasa nimeambiwa kidonda kioshwe kwa dripu la maji ambalo hugarimu sh.2,500/=kila baada ya siku moja na fedha hiyo mama yangu hana ,maana anamzigo mkubwa wa kuniuguza mimi”amesema Mwajuma.

  Kwa upande wake Fatuma Bashiru ambaye ni mama mzazi wa Mwajuma Mfaume alisema kuwa amehangaika na mwanaye katika kufanikisha matibabu kwa kuomba misaada mbalimbali lakini hawajafanikiwa .

 Fatuma amesema kuwa waliwahi kupata kibali cha mtendaji wa kata ya Lizaboni kilichotolewa Novemba 27 mwaka huu ambacho alimwambia apite kuomba kwa wafanyabiashara wa maduka jambo ambalo alishindwa kutokana na kukosa muda wa kufanya hivyo.

 Aidha katika hatua nyingine amewataka watu wenye kuguswa na hali ya mwanae basi waweze kumtafuta kwa namba ya simu ya kiganjani ,0653-543498 ambayo alisema anapatikana hata kwa kumpigia katika kumtia moyo.

                   
Share To:

Francis Godwin Mzee wa matukiodaima

Post A Comment: