Basi jipya lililonunuliwa na kwaya ya Yeriko 
katibu wa Siasa na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Njombe Erasto Ngole akiwa na 

katibu wa Siasa na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Njombe Erasto Ngole akitoa hotuba yake 
Kwaya  ya wito, Kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania (KKKT) mtaa wa Yeriko ,usharika wa Idunda dayosisi ya kusini yanunua basi kwa shilingi milioni 59 kwa ajili ya kueneza  injili .mwandishi  Maiko Luiko  kutoka Njombe .

Huku katibu wa Siasa na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Njombe Erasto Ngole akiwachangia kiasi cha Tsh milioni 1.3

"lengo la kukusanya Fedha kiasi cha Tsh, Milioni 14 ili kumalizia Deni lililobaki kati ya Tsh, Milioni 59 ambazo zilikuwa zikihitajika ili kukamilisha Ununuzi wa Basi hilo"


Akisoma risala ya ununuzi wa basi hilo wakati wa harambee ya kuchangia fedha za kumalizia deni la basi hilo ,Atukuzwe Mbwilo alisema  licha ya mafanikio waliyoyapata ya kununua gari hilo na vyombo vya muziki, bado wanakabiliwa na Changamoto ya ukosefu wa mfadhiri atakaeweza kusimamia huduma yao ya Uimbaji.

Shughuli ya harambee na uzinduzi wa basi la Kwaya ya Wito iliyofanyika katika Kanisa la kanisani hapo ilihudhuriwa  askofu wa Dayosisi ya kusini Dkt, George Fihavango ambae kwa niaba ya Waumini walioshiriki tukio hilo.

Pamoja na kuwapongeza waumini na mgeni rasmi kujitolea fedha katika harambee hiyo pia aipongeza kwaya hiyo kwa ununuzi wa basi hilo na kuwa ni hatua kubwa kwa kazi ya kueneza injili ndani na nje ya dayosisi hiyo .


Kwa upande wake Katibu wa Siasa na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Njombe Erasto Ngole aliyekuwa  mgeni rasmi kwenye harambee ya kuchangia ununuzi wa basi hilo pamoja na kuwapongeza wanakwaya hao bado aliwataka kuwa kioo katika uimbaji .

Ngole aliwataka kuchukua na kuyafanyia kazi baadhi ya mambo mazuri yanayofanywa na vikundi vingine vya kwaya mkoani hapa ili kulitangaza neno la Mungu kwa Ukamilifu.

Alisema  Kwaya hiyo imefanya jambo jema ambalo linatakiwa kuigwa na Kwaya nyingine Mkoani Njombe, kwani basi hilo licha ya kutumika kueneza Injili kwa njia ya Uimbaji pia litatumika kama Chanzo cha Mapato ya kwaya pindi inapobidi kufanya hivyo.


Katika kuwaunga mkono waimbaji wa Kwaya hiyo Ngole aliwaunga  mkono kwa kuchangia shilingi  1.3 ili  kuchangia sehemu ya deni la  ununuzi wa basi hilo ambalo tayari Kwaya ya wito imekabidhiwa kutoka dukani.

Katika harambee hiyo kiasi cha shilingi milioni 18 zilipatikana   huku uongozi wa Kanisa na Kwaya hiyo  ukiomba wadau kuendelea kuchangia ili kupata kiasi cha Tsh, Milioni 25 ili kuweza kukamilisha marekebisho ya gari hilo ikiwemo kulipa bima.

Share To:

Francis Godwin Mzee wa matukiodaima

Post A Comment: