Tuesday, 10 December 2019

Abiria washindwa kujizuia haja kwenye basi la Fikosh


                      PICHA YA MAKTABA


Mwandishi wetu.
Abiria waliokuwa wanasafiri katika basi  la Fikoshi Investment lenye namba CJQ 872 kutokea Iringa kwenda Mwanza,wameshindwa kuzuia haja wakiwa katika basi  wanalosafiria.

Inaweza ikaoneka kuwa ni stori ya kusimuliwa lakini ndio hali halisi wanayokumbana nao wasafiri wanaotumia usafiri wa mabasi ya kwenda mkoani.

Tukio hilo limetokea hivi leo ambako chanzo cha baadhi ya abiria hao kujisaidia ndani ya basi ni dereva aliyekua anaendesha gari hilo kukataa kutoa msaada wa kuchimba dawa njiani wakati wakiwa njiani kuelekea Dodoma

Imedaiwa na baadhi ya watu kuwa si mara ya kwanza kwa abiria kujikuta wanashindwa kujizuia kujisaidia ndani ya basi hilo, kutokana na dereva na kondakta wa  basi hilo kuwa na lugha kali kufikia kuwatisha wateja wao kuomba dharura inapotokea

"Dereva amekua akitoa sababu ya kupigwa faini lakini wakati huohuo ni bora wasimame wachukue wateja na si kutoa msaada kwa wateja wao.,"Hili gari lilivyo kwanza hawana utaratibu wa  vituo vya kuchimba dawa ukitoka Iringa unaambiwa gari litasimama dodoma hotelini na mwendo kutoka dodoma stendi hadi hoteli wanayodai ni kama lisaa limoja na dakika kumi,na ukiomba lazima utajibiwa vibaya,"Msafiri

"Mimi juzi nilitoka nalo Mwanza wamekuja kutusaidia Singida wateja wamelalamika lakini walikuwa wanajibiwa vibaya,si mara moja watu kujisaidia haja tena watu wazima,"Alisema John Makoya

"Hapa tupo kwenye gari,linanuka mikojo watu wanaumia na kuhaibika,dereva yeye anachojua ni kuwahisha gari lifike mapema lakini wanasahau kuwa haja haigongi na haivumiliki," alisema mmoja wa msafiri

"Tunaomba  serikali iliangalie hili suala la vituo vya kuchimba dawa njiani maana madereva wamekua wakitoa sababu ya faini lakini kwa hali ya ubinadamu huwezi kubana haja ndogo ama kubwa na hili nililoshuhudia leo kuna haja ya kusaidia wasafiri," alisema Amina Ally

"Wamiliki wa mabasi wajitahidi kuangalia watu wanaowaajiri,madereva wa mabasi na makondakta wamekua na lugha kali kwa abiria wao yaani kama vile watu hawalipi nauli wamepakia bure,'" Amina Ally

No comments:

Post a comment