Thursday, 21 November 2019

Wimbo UNO wa msanii Harmonize Wafutwa Youtube

Wimbo UNO wa msanii Harmonize umeondolewa kwenye mtandao wa YouTube baada ya mtayarishaji Magix Enga wa nchini Kenya kudai kuwa Harmonize ameiba Beat katika  wimbo aliotayarisha uitwao Dundaing wa King Kaka feat. Kristoff.

Novemba 17, 2019  Enga alimuomba Harmonize kuufuta wimbo huo katika mtandao huo na kumpa wiki moja na kuahidi kuwa asipofanya hivyo, atachukua jukumu hilo mwenyewe.

Kupitia ukarasa wake kwenye mtandao wa Instagram, Magix ameandika;  “Week Imeisha and The song Uno is no longer on YouTube Don’t sample magix Enga Beats. I repeat, dont! Like I said i’m not going to allow this to happen not in 254 🇰🇪.”

No comments:

Post a comment