Mbunge wa Jimbo la Buyungu,Wilayani Kakonko Mkoani Kigoma Mhe.Aloyce Kamamba amehoji juu ya usawa uliopo kati ya Mwanafunzi wa Kike na Kiume chini ya Sera ya Elimu isemayo mwanafunzi akikaa nje ya shule kwa Siku 90 tayari ameshajiondoa kwenye Mfumo wa Elimu.
Ambapo amehoji "Sera hiyo haitoi haki sawa kwani wanafunzi wa kike wanaopata mimba wakiwa shuleni wameruhisiwa kurudi huku wanafunzi wa Kiume wanaopata changamoto mbalimbali na kushindwa kuhudhuria masomo kwa siku 90 wanafutwa kwenye Mfumo wa Elimu ,Je usawa upo wapi wakati yule wa kike anakaa zaidi ya miezi tisa nyumbani?
Pia Mhe.Kamamba ameitaka wizara ya Elimu kuja na Takwimu juu ya wanafunzi wangapi wamepata ujauzito wakiwa Shuleni na kurudi tangu Mhe.Rais Dkt.Samia aliporuhusu hivyo.
"Pia nataka kufahamu hizo changamoto zinazowakumba hao wanafunzi mpaka wanapata Ujauzito mnazishughulikiaje? ,"Ameuliza Mhe.Kamamba Wakati akichangia Mjadala wa Bajeti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia leo Mei 16,2023 Bungeni Jijini Dodoma
Na Mwandishi Wetu, DAR
MSANII wa muziki wa kizazi kimya nchini Benard Paul ‘Ben Pol’, ni miongoni mwa wasanii 10 wa Afrika walioimba kwa pamoja wimbo maalum wa kujilinda na maambuzi ya virusi vya corona vinavyosababisha ugonjwa wa COVlD19.
Akizungumza na tovuti hii, Ben Pol amesema kwamba wimbo huo unaitwa Stand Together, ambao ameshirikiana na 2face Idibia wa nchini Nigeria), Ahmed Soultan wa Morocco, Teni na Yemi Alade wa Nigeria na Amanda Black wa Afrika Kusini.
Ben Pol amesema wasanii wengine alioshirikiana nao n iStanley Enow wa Cameroon, Gigi LaMayane wa Afrika Kusini, Prodigio wa Angola na Betty G wa Ethiopia, lengo likiwani kuhamasisha Afrika nzima kuendelea kujikinga na kutopata maambuziki ya ugonjwa huo ambao umekuwa tishio kila nchini.Pol alisema kuna baadhi ya nchini za Afrika zina ukaribu wa kuingia nchi moja baada ya nyingine hata baadhi ya familia kujumuika pamoja, ambapo sasa imekuwa tofauti, ambapo kila mmoja anahitajika kumuelemiusha mwingi ne ili ugonjwa huo uondoke Afrika na dunia kwa ujumla.
“Tumefanya wimbo huu lengo ni kuhamasisha Afrika nzima, kuendelea kuchukua taadhari , kila mmoja wetu aendelee kuhamasisha ikiwa ni pamoja na kujilinda na kuwalinda wengine, wajiepushe na Corona”alisema Ben Pol.
Aidha Pol alisema kuwa kuna baadhi ya nchini barani Afrika bado wana tatizo kubwa na wananchi wake kupatwa na maambuziki ya ugonjjwa huo.

Kupitia ukarasa wake kwenye mtandao wa Instagram, Magix ameandika; “Week Imeisha and The song Uno is no longer on YouTube Don’t sample magix Enga Beats. I repeat, dont! Like I said i’m not going to allow this to happen not in 254 🇰🇪.”
Kiba amewataka Watanzania wamsapoti Diamond Platnumz kwani ni msanii mzuri na anaiwakilisha nchi vizuri
Kiba amesema hayo katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika Novemba 8, jijini Dar es Salaam ambapo amesema hana ugomvi na Diamond isipokuwa alishamwambia hatoshiriki onesho lolote atakaloandaa
“Diamond nilishamwambia sitoweza kushiriki katika onesho lolote atakalofanya, nafurahia mafanikio anayopata, kama amepata siwezi kufanya kwasababu mimi pia nina yangu ya kuyafanikisha, hakuna ugomvi kati yetu
“Nilipomjibu nikitumia mfano wa penseli nilimaanisha kuwa aache mambo ya kitoto kwasababu nilishamjibu, mimi sio mtoto mdogo sirudii tena kujibu, mimi mwanaume na mwanaume anaongea mara moja tu
“Nafurahia sana muziki wa Diamond naomba muendelee kumsapoti kwasababu ni msanii mzuri, anafanya kazi nzuri na anawakilisha nchi yetu,” amesema Kiba.
"Alikiba Unforgettable Tour itakuwa na mambo makubwa matatu. 1. Ujenzi wa Ndoto kazi kwa vijana, ambapo mimi na wenzangu watakaonishika mkono tutapita mikoani kuzungumza na wanafunzi wa vyuo. Jambo namba 2 kwenye Alikiba Unforgettable Tour ni Medical Camp, hapa namshukuru Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu na jopo la madaktari, ambao watatoa mchango wa dawa kwa lengo la kutoa huduma ya afya kwa watu mbalimbali bure kabisa.", ameongeza.
Tamko hilo amelitoa leo Novemba 8, 2019, baada ya Kamati ya Uongozi wa Chama hicho na kuagiza ile asilimia 4 ya wagombea wote waliopitishwa, wajiengue kushiriki katika uchaguzi huo kwa kuwa haki haijaweza kutendeka.
"Sisi hatutashiriki kwa sababu tumeondolewa, toka juzi tumekuwa na mashauriano na vyama vya siasa nchini, wenzetu wametoa maamuzi yao jana, sisi tumetoa maamuzi yetu leo, tutawajulisha wananchi hatua gani tutaenda kuchukua kwa ajili ya kulinda kilicho chetu, wao wametuondoa asilimia 96 na sisi tumewasaidia kuiondoa ile asilimia 4 ili tusishiriki kabisa" amesema Zitto.
Jana Novemba 7, 2019, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kilitangaza rasmi kutoshiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, siku ya Novemba 24, ambapo pia kiliwataka wagombea wake walioenguliwa kutokata rufaa.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk.Bashiru Ally Kakurwa, Leo, Amemkabidhi Komredi Yohana Lukosi Anayefanya Kazi katika Ofisi za Makao Makuu ya CCM Yaliyopo Jijini Dodoma, Cheti cha Mfanyakazi Bora wa Chama Hicho kwa Mwaka Huu Pamoja na Kitita cha Fedha Shilingi Milioni Moja Ambapo Laki Tano Iliyotolewa na Chama Hicho na Laki Tano Nyingine Kuchangiwa na Viongozi Waliohudhuria katika Shughuli Fupi ya Makabidhiano ya Cheti Hicho.
Akizungumza Baada ya Kutoa Cheti cha Ufanyakazi Bora wa Mwaka 2019 iliyokwenda kwa Mfanyakazi Huyo,Katibu Mkuu wa CCM,Dk.Bashiru, Aliipongeza Kamati Maalumu ya Uangalizi wa Utendaji Kazi wa Wafanyakazi kwa Kumaliza Vizuri Mchakato Huo Ambapo Alisifia na Sifa na Vigezo Vilivyomsababishia Komredi Yohana Lukosi Kuwa Mshindi wa Mfanyakazi Bora kwa Mwaka Huu kwa CCM, Alisema Kwa Sifa Alizozipata za Utendaji Kazi wa Mtumishi Huyo wa Chama Alistahili Kupata Ushindi Huo na Kuwataka Watumishi Wengine Kuiga Mfano Wake.
“Sisi Sote Tumesikia Sifa Zilizofanya Mtumishi Mwenzetu Kushinda Kuwa Mfanyakazi Bora kwa Mwaka 2019 Tulipaswa Shughuli Hii Tuifanye Tangu Mei Mosi katika Sikukuu ya Wafanyakazi Ila Kutokana na Majukumu Yetu Tulipeleka Mbele Hatimaye Leo Tumemtunukia Mwenzetu Cheti cha Ufanyakazi Bora Pamoja na Sh.500,000 kutoka Chama na Mimi na Viongozi Wenzangu Hapa Mbele Tukamchangia Hadi Kufika Sh.Milioni Moja,Niwaombe Watumishi wenzangu Tuige Mfano wa Utendaji Kazi wa Komredi Yohana Lukosi;
“Yapo Mambo ya Muhimu yaliyoasisiwa na Tanu na Asp Ambayo Hadi Sasa CCM Lazima Tuyahifadhi Mfano kwa Kumbukumbu ya Ukumbi Huu Hata Kama Mchumi Wetu Anataka Fedha Hatuwezi Kuubadilisha Ukumbi Huu wa White House Kuwa Kumbi ya Starehe Eti Kisa Tunaingiza Fedha, Ila Kuna Mambo Ya Kubadilika Kulingana na Hali Ilivyo,Chama Chetu Kwa Sasa Tupo Vizuri Kiuchumi Hii Inatokana na Utendaji Kazi Wenu Ninyi Ndugu Zangu Watumishi” Alisema Katibu Mkuu, Dk.Bashiru.
Aidha Dk.Bashiru Aliwaambia Watumishi Hao Kujitoa kwa Moyo Wote katika Kuhakikisha CCM Kinafanya Vyema Utendaji Kazi Wake Ili Kiendelee Kushika Hatamu,Alisema Hata Kama Mfanyakazi Akilipwa Mshahara Mkubwa Ila Asipokuwa na Moyo wa Kujitolea Hakuna Kitakachoendelea kwa Hilo Nawapongeza Sana Wanachama Wenzangu wa CCM Tunazidi Kusonga Mbele na Kuzikabili Changamoto Zetu,Tuzidi Kufanya Kazi kwa Bidii Mabadiliko Yatakuja Tu Kama Si Leo Basi Kesho.
Pia Katibu Mkuu Huyo Aliwakumbusha Wanachama Hao Kujiendeleza katika Elimu Ikiwezekana Mfanyakazi Akajiendeleze Kulingana na Kazi Zao Akatolea Mfano Dereva wa Kawaida Akienda Kusomea Jinsi ya Kuendesha Viongozi (VIP) Itampa Ufahamu wa Namna Bora ya Utendaji Kazi Wake, Alitoa Maagizo kwa Chama na Jumuiya Zake Ziandae au Ziwasomeshe Watumishi Wake Kwa KUwa Elimu Haina Mwisho,Alitoa Mfano Akisema Ikitokea Dereva Akataka Kwenda Kufundishwa Kupika Chakula Kizuri Hatogharamia Kila Mtumishi wa CCM Ingependeza Asomee Kile Anachokifanyia Kazi.
Akitoa Salamu katika Mkutano Huo,Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara,Rodrick Mpogolo,Alimuambia Katibu Mkuu, Dk.Bashiru Kuwa Wamejipanga katika Kuhakikisha Chama Hicho Kinashinda kwa Asilimia 100% katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa,Vitongoji na Vijiji Kutokana na Utekelezaji Mzuri wa Serikali ya Awamu ya Tano Inayotokana na Chama Hicho Inayosimamiwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais,Dk.John Pombe Joseph Magufuli.
Mkutano Huo Pia Ulihudhuriwa na Makatibu Wakuu wa Jumuiya Zote za Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ambao ni Katibu Mkuu wa Umoja wa Wazazi Tanzania,Erasto Sima,Katibu Mkuu Uvccm,Mwalimu Raymond Mwangala,Katibu Mkuu wa UWT,Mwalimu Queen Mlozi na Viongozi Wengine.
Mwishoo
0719976633.










