Monday, 11 November 2019

LUKUVI ATOA MAAGIZO NDANI YA SIKU 90 WAKAZI 1430 WA NZUGUNI WAWE WAMEPATIWA HATIMILIKINYA ARDHI


Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma

Waziri wa   ardhi,nyumba na Maendeleo  ya Makazi,Mhe.Wiliam Lukuvi ametoa maagizo ndani  ya Miezi 3 kwa jiji la Dodoma kuhakikisha wananchi 1430 walio kwenye  Mgogoro wa Ardhi mtaa wa Nzuguni wawe
wameshapatiwa hatimiliki za za ardhi katika eneo hilo.

Akizungumza na wananchi  leo Nov.10,2019  Waziri Lukuvi amesema Serikali ya awamu ya Tano haitakubali wananchi wa kawaida wanaporwa ardhi iwapo wanaishi kiuhalali katika maeneo hayo huku akiwataka kufuata maelekezo ya mipango miji na kusisitiza kuacha kuanzisha majengo bila kibali cha ujenzi.

Aidha,Waziri Lukuvi amesema Wizara yake itaendelea kumlinda mtu mwenye hatimiliki  ya ardhi huku akiwaasa wananchi kufuata kanuni na taratibu za ulipaji wa pango la ardhi.

Awali kabla ya kutoa Maagizo hayo Waziri Lukuvi alisikiliza kero kutoka kwa mwananchi Mmoja baada ya Mwingine ambapo  wananchi wa Nzuguni walitoa Malalamiko yao .

Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi imekuwa Mstari wa Mbele kutatua Migogoro  mbalimbali ya ardhi  hapa nchini kupitia Kampeni ya funguka kwa Waziri.
.

No comments:

Post a comment