Saturday, 16 November 2019

JESHI LA POLISI TARIME RORYA LAWASHIKULIA VIJANA WATANO KWA TUHUMA ZA MAUAJI


Na Frankius Cleophace Tarime.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Polisi Tarime Rorya linawashikilia vijana watano kwa tuhuma za mauaji ya Mwalimu aliyejulikana kwa jina la  Justine Sospeter Ogo  aliyekuwa anafundisha shule ya Sekondari Itiryo

Kamanda wa Polisi Tarime Rorya SACP Henry Mwaibambe amewataja vijana hao kuwa ni Nchore Richard, Marwa Mwita Gichome, Kisiri Simon Mhere,Makenge Honga Chacha na Mohere Mwita Gichemu.

Mwaibambe amesema kuwa chanzo cha mauaji hayo ni vijana wapatao 8 wakiwa wanatembea barabarani  wakiwa na silaha za jadi huku wakijiandaa na Tohara ambayo inatarajiwa kufanyika Desemba Mwaka huu, ambapo mara nyingi vijana hao uwasimamisha watu nakuomba fedha  kwa nguvu ili kuonyesha ujasiri.

Ndipo sasa Marehemu alikuwa anampeleka Mwalimu Mwenzake  kusimamia mitihani  ya kidato cha Nne shule ya sekondari Bungurere na vijana hao walimsimamisha nakuanza kumwomba pesa huku walimu wenzake wakiendelea na safari bila kusimama na ndipo kijana mojawapo alimchoma mshale shingoni kutoka upande wa kulia na kutokea upande wa kushoto na alifariki kipindi akipelekwa hospitali.

Kamanda ametoa Mwito kwa  wananchi wote kuwafunza watoto wao maadili mema na kamwe sheria haitaacha kamwe kuwachulia sheria kali watoto wote wanaofanya uharifu huku akisema kuwa umri wa vijana unachunguzwa.

No comments:

Post a comment