Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika wiki ya asasi za Kiraia Tanzania  [AZAKI]itakayofanyika jijini Dodoma kuanzia Novemba 4-8,2019.
 
Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dodoma leo Oktoba 31,2019,Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Foundation for Civil Society  [FCS]BW.Francis Kimwanga amesema wiki ya asasi za kiraia nchini itakutanisha zaidi ya asasi za kiraia 500 kutoka nchi nzima Tanzania bara na visiwani Zanzibar.

Mkurugenzi mtendaji huyo wa  FCS]  amefafanua kuwa Wiki ya Asasi za Kiraia [AZAKI]itajumuiya Maonesho  ya kazi mbalimbali zinazofanywa na asasi hizo huku lengo likiwa ni kuimarisha ubia kati ya asasi za kiraia na wadau mbalimbali  katika kutimiza azma ya kuiletea Tanzania Maendeleo.
 
"Lengo la kongamano hilo nikuimarisha ubia kati ya asasi za kiraia na wadau mbalimbali katika juhudi za kutimiza azma ya kuileteaTanzanaia maendeleo," amesema .

Hata hivyo amesema "Kupitia  kongamano  hili asasi  za  kiraia  zitafanya majadilianao juu ya kazi  zao, kubadilishana uzoefu na kuona ni jinsi ambavyo zinaweza kushirikiana wenyewe kwa wenyewe na wananchi, serikali, bunge, wabia  wa  Maendeleo na sekta binafsi," amesema.

Kwa upande wake Mbunge wa Viti  maalum mkoa  wa Dodoma  Fatma Taufiq ambaye  pia  ni  Mkurugenzi wa shirika  la  WOWAP  amesema wiki hiyo  ni  Wiki  ya kipekee  kwa  mwaka  huu washiriki  mbalimbali  wanatarajiwa kuwepo bila  kuwasahau viongozi  wakubwa kutoka serikalini huku pia akitoa rai kwa vyombo vya Habari kuhabarisha jamii umuhimu wa makundi maalum katika jamii.
 
“Asasi za kiraia zimekuwa na mchango mkubwa katika jamii,AZAKI inatekeleza Malengo 17 ya maendeleo endelevu hivyo nitoe rai kwa asasi ambazo zimekuwa zikienda kinyume na matakwa ya serikali na asasi sio adui zinashirikiana  na serikali .Pia nitoe rai kwa Vyombo vya Habari kuhabarisha umma juu ya Umuhimu wa Asasi hizi.amesema.

Hata hivyo  aliwataka  wananchi  wote kufika  katika viwanja  vya Jamhuri Novemba 4 Hadi 8 ili  kuweza  kuona  na  kujifunza  asasi  za  kiraia zinafanyaje  kazi zao n'a kuachana na  kusikiliza  habari  potofu kuwa  asasi za kiraia zinakula  hela na hazileti Maendeleo yoyote huo ni upotoshaji.

Msajili wa  asasi za kiraia kutoka Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,jinsia Wazee na Watoto,Charles Komba amesema asasi za kiraia zimekuwa chachu kubwa ya Maendeleo  na katika kuisaidia serikali.
 
“Asasi za kiraia ni Wadau wetu,ni wadau  wetu wakubwa   sana katika maendeleo ya kijamii,serikali haiwezi kufanya kwa kila jambo lakini sasi za kiraia zmekuwa mstari wa mbele kutusaidia.
 
Aidha,ameongeza kwa kusema ,Mpaka  mwaka 2017 serikali ilishasajili asasi za kiraia zaidi ya 10,000.

Mkurugenzi Mtendaji wa  Taasisi ya Haki,Rasilimali ,Mafuta ,Madini na gesi Rachel Chaganda amesema  taasisi hiyo imekuwa mstari wa mbele katika kufanya tafiti mbalimbali zinazohusiana na madini,Mafuta na gesi ambapo ni mchango mkubwa kwa serikali  Ya Tanzania.

Naye mwenyekiti wa Shirikisho la Wenye Ulemavu Tanzania[SHIVYAWATA] Ummy Nderiananga amesema katika wiki hiyo ya AZAKI,Kutakuwa na elimu pamoja na miradi mbalimbali  inayofanywa na watu wenye ulemavu huku afisa Uhusiano wa kituo cha sheria na Haki za Binadamu,Legal Human Rights   Centre[LHRC] Michael Malya akisema katika wiki hiyo kituo hicho kitajihusisha na utoaji wa huduma za kisheria.
 
Ikumbukwe kuwa FCS itatoa tuzo za Umahiri wa asasi za kiraia  ili kusheherekea na kutambua ufanisi na michango   za taasisi na watu binafisi  katika uchocheaji na uimarishaji wa sera ya maendeleo ya nchi.
 
Zaidi ya asasi za kiraia 15  zikishirikiana na FCS   Kuandaa wiki ya AZAKI ni LHRC,LSF,Save the children, Wajibu Institute,UN Women,Oxfam,Twaweza,Policy Forum,msichana Initiative,Hakirasilimali, UNA Tanzania, Acountability Tanzania,Sikika,TLS,SHIVYAWATA,na TANGO.
Kaulimbiu  wiki  ya asasi za Kiraia [AZAKI] Mwaka ,2019 ni ubia kwa Maendeleo ,Ushirikiano kama chachu ya Maendeleo.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: