Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi amewataka wakazi wa mkoa wa Singida na mikoa mingine kujitokeza kwa wingi katika maadhimisho ya siku ya chakula duniani yanayofanyikia kitaifa mkoani hapo ili kupata elimu ya lishe bora na kilimo chenye tija ili kuepukana na njaa kitaifa na Dunia kwa ujumla.

Ameyasema hayo hivi leo alipotembelea kukagua maandalizi ya maadhimisho hayo yaliyoanza rasmi hivi leo mkoani hapo katika viwanja vya Bombadia(Peoples Power)ambapo ndipo maonyesho hayo yanapofanyikia.

Nchimbi amewataka wakazi wa singida kuiona fursa waliyoipata ya maonyesho hayo kupangwa kufanyikia mkoani hapo na kuitumia kwa kutembelea mabanda kwaajili ya kupata elimu afya na lishe bora kwa ujumla na kujionea fursa zilizopo katika kilimo pia.

Amesemakuwa endapo watatembelea watapata fursa ya kujionea vyakula lishe na kujifunza namna bora ya kuandaaa na kulima mazao lishe ili kuepukana na njaa katika jamiii yao na kwa dunia kwa ujumla.

‘’unapopata fursa ya kuja au kusikia taarifa hizi hakikisha unamjulisha na mwenzako kwani hiii ni fursa kubwa sana ninaimani hapa pia wajasiriliami wadogo wadogo  kupitia maonyesho haya watapata elimu na  fursa ya kuuza bidhaa zao’’alisema Dkt Nchimbi.

Akizungumzia hali ya maandalizi ya maonyesho hayo amesemakuwa mpaka sasa maandalizi yamekamilika na  muitikio ni mkubwa kwa wananchi wa mkoa wa Singida na mikoa ya jirani kwani kwa siku ya kwanza tu wananchi wameonyesha kuvutiwa na maonyesho hayo kwa kujitokeza kwa wingi katika viwanja hivyo.

Maonyesho hayo ya siku ya chakula Duniani kitaifa mkoani Singida  yameanza hivi leo tarehe 10 na yanatarajiwa kuzinduliwa rasmi tarehe 12 na kuhitimishwa tarehe 16 ambapo ndio siku ya kilele,ambapo mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) yakiwa na kaulimbiu ya ‘’lishe bora kwa ulimwengu usio na njaa’’
Share To:

msumbanews

Post A Comment: