IMG_20191031_134701.jpeg
MKURUGENZI wa Halmashauri ya Jiji la Arusha Dk.Maulid Madeni amesema halimashauri hiyo, haitalipa Sh.bilioni 1.9 za fidia kwa wananchi wa Kata ya Olasiti katika eneo la Mradi wa kituo cha Mabasi baada ya kunusa harufu ya ufisadi.

Aidha amewaonya baadhi ya watumishi wa halmashauri wanaotumika kuhujumu halmashauri hiyo kwa maslahi binafisi na kuandaa mabango ya maandamano kwa wananchi ambao wamekubali kupisha mradi huo.

Aliyasema hayo katika kikao cha kawaida cha Baraza la Madiwani,baada ya kulazimika kutoa ufafanuzi kufuatia baadhi ya wananchi wa kata hiyo kutumiwa vibaya na mafisadi hao na kuandamana wakishinikiza kulipwa fidia kiasi hicho cha fedha badala ya sh,bilioni 1.15 zilizopo kwenye makubaliano.

Dk.Madeni alisema kwa taarifa alizonazo eneo hilo la ekari 29.5 la Olasiti limenunuliwa na watu wawili ambao wanashinikiza wananchi waandamane ili walipwe fidia hiyo.

"Kweli siko tayari kulipa watu wanaofanya ufisadi kwa kujifunika blanketi la ufisadi, wajuwe sasa limetoboka na hii vita dhidi ya mafisadi na waaminifu,maana kuna watu wanakula fedha halali kwa njia ya kifisadi,"

" Hiyo milioni 800 ni bora tukajenga shule nyingine mpya kuliko iingie kwenye midomo ya mafisadi wachache ambao bado wapo wanatusumbua Amesema Madeni

Alisisitiza kuwa mafisadi wanatumia njia haramu kupata fedha halali ama wanatumia njia halali kupata fedha haramu,..alisema akiondoka kwenye nafasi yake kwa kutenda makosa atajutia ,ila nikiondoka kwa kusimamia vema fedha za JPM nitakuwa shujaa.

Alisema wanachokifanya wananunua ekari moja kwa Sh.milioni 10 alafu wanauzia halmashauri Sh.milioni 80 au 100, bei ambayo haipo popote nchini na hatakaa kuikubali.

Aidha alisema hawezi lipa fedha hizo kwa kupitia mapato ya ndani ambazo zinaenda kwa mafisadi hao na kuacha kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo,hata hivyo alisisitiza kuwa bei atakayowalipa ni sh,Milioni 40 kwa kila hekari moja na si vinginevyo.

"Kama sasa hivi tunajenga hospitali ya wilaya kwa Sh.milioni 800 kwa kutumia fedha za ndani eti niache nipeleke kulipa mafisadi sikubali na katika hili niko tayari hata kama kusimamia fedha za Rais Magufuli zisiliwe basi nifukuzwe kazi kama wanavyotaka na kunichafua sawa niko tayari kwa kuwa nasimamia haki,"alisema na kuongeza:

"Katika sakata hili utaona wazi ufisadi ulivyo wazi maana katika muhtasari wa 24.2.2017 unasema walipwe fidia ya Sh.bilioni 1.1 lakini mwaka huo huo ukaandikwa muktasari 6.3.2017 kwenda Tamisemi wakiomba kibali cha kuchukua mkopo benki ya NMB wa Shbilioni 1.15 sasa hii iliona wapi duniani kama sio ufisadi,"alisema

Alisisitiza Stendi itajengwa eneo la Bondeni City ambako wamepata eka 30 bure na kuokoa fedha hizo ambazo zitaenda kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo.

Alisema amewashangaa mafisadi hao kutumia wananchi wanyonge na kuwaachisha mama nitilie kupika siku hiyo kwa kuwashikisha mabango ya kuandamana kushinikiza kulipwa fidia wakati sio wakazi wa eneo hilo na matokeo yake waliwatumikisha katika mbinu zao chafu kwa kuwapa ujira wa Sh.10,000.

"Mimi sitishiki na mafisadi ambao naamini bado wapo kwenye chama na halimashauri na nitaendelea kupinga ufisadi wa kiharamia unaofanyika katika Jiji hili na baadhi ya watu,"alisema.

Naye Naibu Paul Matthysen baraza hilo halitishwi na linaheshimu maadhimio yake kuwa stendi kubwa ijengwe Bondeni City na hawatabadili msimamo wao kwa maandamano.

Alisema wao halmashuri waliingia ubia na Bondeni City nwaka 2015 na kupata eneo la ekari 30 ambalo gharama kubwa kama hizo hakuna.

"Sasa hakuna mtu atakayekubali kuacha eneo lenye unafuu tukaenda kwenye Bilioni 1.9 labda kichaa na hakuna wa kuingilia maamuzi yetu sisi watu makini,"alisema

Aidha alimpongeza mkurugenzi Dk.Madeni kufanikisha kupatikana kwa eneo hilo na kuwaonya mafisadi wanaomchafua Mkurugenzi huyo kwa maslahi yao kuacha mara moja kwani hawatafanikiwa na wao hawarudi nyuma.

Diwani wa Kata ya Ngarenaro Isaya Doita alisema hakuna haja ya kujadili suala hilo ambalo walishapitisha maadhizio yao sababu kuendelea kulizungumza sawa na kuotesha mbegu juu ya jiwe.

Kabla ya kikao hicho Oktoba 30 mwaka huu wananchi wa Mtaa wa Oloresho Kata ya Olasiti zaidi ya 80 waliandamana wakiwa na mabango, wakipinga mradi wa ujenzi wa stendi kubwa kuhamishiwa eneo la Bondeni City,huku wakiliacha eneo lao la ekari 29.5 lililotengwa mwaka 2012 katika Kata ya Olasiti, ambalo lilipitishwa kujengwa stendi hiyo na kuamriwa kulipwa fidia kwa wananchi wa eneo hilo.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: