Tuesday, 29 October 2019

Miss World Atembelea Hifadhi Ya Taifa Ya Arusha


Na Ferdinand Shayo,Arusha

Miss Dunia Silvia Vanessa ametembelea Hifadhi ya taiga ya Arusha (ANAPA) ambapo amejionea makundi ya wanyama mbalimbali ikiwemo twiga,nyumbu pamoja na aina za ndege walioko katika ziwa Momela.

Akizungumza Mara baada ya kutembelea hifadhi hiyo ameeleza kufurahishwa na vivutio adhimu vilivyopo katika hifadhi hiyo  ambavyo ni vya asili na kuzitaka nchi mbalimbali kutembelea hifadhi za Tanzania ambazo zinaongoza kwa vivutio Vingi na mazingira ya asili.

Aidha ameeleza kuvutiwa na nchi ya Tanzania na pia anatarajia kurudi nchini kutembelea vivutio mbalimbali na pamoja na  kuhamasisha utalii wa vivutio hivyo.

Miss Tanzania 2019 ,Silvia Sebastian amesema kuwa ziara ya miss Dunia inalenga kutangaza Tanzania na kutangaza utalii kwa ujumla pamoja na kufanya shuguli za kijamii.

 Afisa Mhifadhi Utalii   hifadhi ya taifa ya Arusha Jerome Ndanzi amesema kuwa wamefurahishwa na ujio wa miss Dunia kwenye hifadhi hiyo utasaidia kutangaza hifadhi hiyo kimataifa na kuvutia wageni wengi kuja kuitazama


Kwa Basila Mwanukuzi  ambaye ni Mkurugenzi kampuni ya Goodlook company waandaaji wa Miss Tanzania amesema.kuwa wanafanya juhudi za kutangaza utalii kwa kushirikiana na serikali  katika mpango wa kutangaza Tanzania kimataifa na vivutio vyake.

No comments:

Post a comment