MKUU wa wilaya Korogwe Kisa Gwakisa akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusiana Mashindano ya  Riadhaa ya Korogwe Mini Marathon yanayotarajiwa kuanza kutumia vumbi Octoba 13 mwaka huu mjini humo ambayo yatatumika kumuenzi Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ikiwemo pia kuchangia maendeleo ya wilaya hiyo kulia ni Katibu wa Kamati ya Maandalizi ya Mashindano hayo Juma Mwajasho kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mjini Mary Chatanda na Afisa Tarafa ya Korogwe Michael John

 Katibu wa Kamati ya Maandalizi ya Mashindano hayo Juma Mwajasho  akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Korogwe Kisa Gwakisa,Mbunge wa Jimbo la Korogwe mjini Mary Chatanda na Afisa Tarafa ya Korogwe Michael John


 MBUNGE wa Jimbo la Korogwe Mjini Mary Chatanda akizungumza kwenye mkutano huo kulia ni Mkuu wa wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa kushoto ni Afisa Tarafa ya Korogwe Michael John





 MKUU wa wilaya ya Korogwe Kisa Gwakisa katikati akimkabidhi medali za mashindano hayo Katibu wa Kamati ya Maandalizi ya Mashindano hayo Juma Mwajasho  kulia kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Korogwe mjini (CCM) Mary Chatanda
MASHINDANO ya Riadhaa ya Korogwe Mini Marathon yanatarajiwa kuanza kutumia vumbi Octoba 13 mwaka huu mjini humo ambayo yatatumika kumuenzi Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ikiwemo pia kuchangia maendeleo ya wilaya hiyo.

Mashindano hayo yameandaliwa na Mkuu wa wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa yakiwa na lengo la kuibua na kuendelea vipaji vya vijana wilayani humo ikiwemo kumuenzi Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Mkuu wa wilaya ya Korogwe Kissa alisema kipindi hiki ni muhimu sana kutokana na kwamba watanzania wamempata Rais Dkt John Magufuli ambaye anafafana na Baba wa Taifa ambaye amekuwa akifanya kazi kubwa ya kuwapa watanzania maendeleo.

Alisema lengo kubwa ni kumuenzi baba wa Taifa Nyerere ikiwa ni kutimiza miaka 20 ya kumuenzi lakini pia kuchangia maendeleo wilaya ya Korogwe huku akitoa wito kwa wananchi wajitokeza waungane pamoja kushiriki kwenye mashindano hayo.

“Wakati tunaadhimisha kumbukumbu ya Baba wa Taifa letu sisi Korogwe kupitia Mashindano ya Korogwe Mini Marathon sisi kama Korogwe tutakuwa tumetimiza jukumu letu la kumuenzi baba wa Taifa kwa vitendo”Alisema DC Kissa.

Aidha alisema kwamba watatumia mashindano hayo kuchangisha fedha kwa ajili ya kujenga madarasa 70 ya magufuli ambayo wanahitaji wadau wajitokeza kuwasaidia kwenye harakati hizo za kuhakikisha wanainua sekta ya elimu kwa kuondosha changamoto zilizopo

“Tunawashukuru sana Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) ambaye ni mdau namba moja wamechangia kwenye mashindano haya lakini pia wamewachangia milioni 30 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa nimeona kuna mwamko mkubwa kutokana na mashindano hayo sana lakini pia niwashukuru wadau wengine akiwemo Mwekezaji wa Mkonge Gomba, Klabu ya Sas Cyclne tunaamini kwa mchango wao tutafika mbalimbali sana “Alisema DC huyo

Pia alisema kwamba wamejipanga kuhakikisha kunakuwa na mambo mazuri ambapo kutakuwa na kikimbia kilomita 5 ambapo Mkuu huyo wa wilaya atakimbia ,Kilomita 5 watakimbia pia walemavu kwa kutumia baiskeli na magongo huku akiwaomba wananchi wa Korogwe ambao ni wenyeji lakini nje kuna mwamko mkubwa sana.

Mkuu huyo wa wilaya aliwataka wanakorogwe kujitokeza kwa wingi huku akieleza kwamba wameongea na hifadhi ya Mkomazi ili waweze kupeleka wanyama kwenye mashindano hayo mahali yanapoanzia na yatakapokuwa yakiishia huku akiitaja Hotel ya Rocky Excutive Lodge wamekuwa wadau wakubwa kwenye mashindano hayo.

 Awali akizungumza katika mkutano huo Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mjini (CCM) Mary Chatanda alisema kwamba wao wameunga mkono jambo hilo kwa ni jema wanawatangazia wananchi wajitokeza kwa wingi kwa kufanya hivyo watakuwa wamejitendea haki wenyewe .

Mbunge huyo alisema kwamba jambo hilo ni jema sana kwani kama alivyosema DC ni kupata fedha kwa ajili ya kuchangia maendeeo huku akiwataka vijana wajitokeze kwa ajili ya afya zao.

“Niwahamasishe wananchi wa Korogwe mjini wajitokeze kwa wingi lakini pia wajasiriamali wajitokeze kwa wingi waweze kuweka mali zao kwenye mashindano hayo ili waweze kupata kipato kutokana na wanunuzi”Alisema.

Kwa upande wake Katibu wa Kamati ya Maandalizi ya Mashindano hayo Juma Mwajasho alisema kwamba mashindano hayo yatanzia kwenye viwanja vya Chuo cha Ualimu Korogwe na yatapita njia ya Dar- Arusha hadi kwenye mzunguko njia ya kuelekea Handeni na Kurejea yalipoanzia.

Alisema kwamba pia kutakuwa na mashindano ya baiskeli kilomita 60,Kilomita 10 ya kujifurahisha ikiwemo ya riadha ya Kilomita 10  na kiimota 5 ya kukimbia kujifurahisha huku akiweka bayana zawadi zenye thamani ya milioni 2 kwa ujumla zitatolewa na washiriki wote watakaomaliza kilomita 60 na 10 watapata medali.

Hata hivyo alisema kwamba wanategemea kupata washiriki wengi kwenye mashindano hayo ambapo zaidi ya washiriki 500 watashiriki kwenye mashindano hayo huku wengine wakitokea nchi jirani ya Kenya ambao wameunganishwa kupitia Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi.

Mwisho.

Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: