Monday, 9 September 2019

MWITA WAITARA AWASHUKIA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAANA HERI SHAABAN

UCHAGUZI wa Serikali za Mitaa imebaki mwezi mmoja kuanza huku ukiwa umechukua sura mpya,NAIBU Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)Mwita Waitara,amewataka Wenyeviti wa Serikali za Mitaa waliomaliza muda wao ambao walikuwa wakitumia madaraka yao vibaya kwa kashifa za migogoro ya ardhi majina yao yatakatwa hawana sifa katika kuwatumikia wananchi.

Naibu Waziri wa TAMISEMI Waitara haliyasema hayo katika ziara ya Serikali Jimbo la Ukonga kukagua miradi ya Maendeleo sambamba na kusikiliza kero za wananchi.

"Nafasi yenu ya Wenyeviti wa Mtaa ni ya kujitolea  mlichaguliwa na wananchi ili muwatumikie muda wenu umekwisha wale Wenyeviti waliosababisha kesi za migogoro ya kuuza ardhi kiholewa na kutumia madaraka vibaya katika serikali ya amamu ya tano hawana sifa ya kuwa kiongozi majina yatakatwa"alisema Waitara..

Waitara aliwataka chama kupitisha majina yanayokubalika ili wapigiwe kura kwa ajili ya kuja kuongoza wananchi na kushirikiana na kasi ya Serikali ya awamu ya tano hapa kazi tu   kujenga Tanzania ya uchumi wa viwanda.

Aliwataka wananchi wa Jimbo la Ukonga na watanzania kwa ujumla  kushiriki uchaguzi huo na kuchagua kiongozi mwenye sifa atakaye weza kuongoza wananchi na kusimamia miradi ya maendelea na kuchukia rushwa kwani ni adui wa haki.

Akizungumzia kanuni za uchaguzi wa Serikali za mitaa alisema uchaguzi wa mwaka huu 2019 wagombea Wajumbe sita kati ya wajumbe sita wanawake wawili na Wanaume wanne .

"Katika Ofisi ya Serikali ya Mitaa kuna mambo mengi ya kijamii serikaĺi imeliona ili tumeweka wajumbe wawili ambao watachaguliwa na Wananchi kwa ajili ya kushuruisha migogoro yenu , wagombea watarajiwa  nakala hizi zipo kwa Maofisa Watendaji wa kata na Wilayani kwa wakuu wa Wilaya zenu"alisema

Wakati huo huo Waitara alisema Serikali imemaliza mgogoro wa Mpaka wa Magore A kata ya Kivule  Manispaa ya Ilala na Temeke hivyo wananchi wa Magore A kuanzia sasa wanahesabika ni wananchi wa Wilaya ya Ilala sakata la mpaka limekwisha.

Alimwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ilala kutafuta Mtendaji wa Magore  A ili wananchi wa mtaa huo waweze kushiriki uchaguzi wa mtaa mwaka huu 2019 waweze kupata haki za msingi na huduma. za jamiï.

Alisema kama Mbunge wa jimbo la Ukonga na Naibu Waziri wa TAMISEMI mara baada kupata serikali yao Magore A watajengewa zahanati,soko,shule ya msingi,maji na umeme wa REA watapelekewa  ila wachague Wenyeviti wenye chachu ya maendeleo atakayeweza kuwatumikia Wananchi.

MWISHO
Naibu Waziri Waitara jimbo la Ukonga Septemba
09/2019

No comments:

Post a comment