Wajumbe wa Baraza Kuu la  UWT Taifa wamefanya  Kikao cha Kwanza  cha kawaida cha baraza hilo katika Jiji la Dodoma jana tarehe 16/8/2019.

Baraza hilo lililohudhuriwa  na Wajumbe zaidi ya Mia Moja likkongozwa na Mwenyekiti Wa UWT Taifa Mama Gaudentia Kabaka na Mgeni Rasmi Ndg. Humphrey Polepole. Katibu wa NEC Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Taifa.

Katika Hotuba yake Ndg. Polepole alisema kuwa CCM ina imani kubwa na UWT na inaitegemea kura za uhakika za wanawake katika chaguzi zote.

Aidha Ndg. Polepole aliwataka Wajumbe kuendelea kuwasaidia wanawake katika changamoto zao mbali mbali na kuwapa nafasi za uongozi kwa ngazi mbalimbali.
"Ili mipango mingi ya maendeleo iguse maisha ya mwanamke ni vema nao wakashirikishwa katika maamuzi" alisema Ndg. Polepole.

Baraza hilo la kihistoria lilijumuisha wajumbe kutoka Tanzania bara na Visiwani Zanzibar na lilikuwa na agenda kadhaa ikiwemo ya kuongeza wanachama na  uchaguzi wa serikali za mitaa. Ambapo wajumbe kwa pamoja waliahidi nilazima CCM iendeleekushika dola.
"Tutaendelea kufanya kampeni usiku na mchana kayika chaguzi zote ili kukalhakikisha tunashinda" alisema Mjumbe

Akizungumza kwa niaba ya Viongozi wa UWT mama Gaidentia Kabaka aliwashuru  wajumbe kwa ushirikano wanaompatia na kuwasihi waendeee kuwatumikia vyema wanawake wa Tanzania.
"Wakinamama wenzangu tuendelee na ushirikiano na pia tuendelee kuwatumikia wanawake wa Tanzania kwa moyo mmoja" alisema Mama Kabaka.

UWT ni chchu ya maendeleo na wakimama hawa wajumbe wa Baraza la UWT Taifa kutoka Mikoa mbalimbali wamedhamiria kuwatumikia watanzania na kuhakikisha pia CCM Inaendelea kuahika dola.









Share To:

msumbanews

Post A Comment: