Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe ameyafunga Mashindano ya 19 ya michezo ya shule za Sekondari kwa nchi za Afrika Mashariki (FEASSSA) kwa kuahidi kuwa mwakani timu kutoka Tanzania zitaleta upinzani mkali kulinganisha na mwaka huu.

Akizungumza kwenye sherehe za kuhitimisha mashindano hayo zilizofanyika leo  leo katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, Mhe.Mwakyembe amewatahadharisha wenyeji wa mashindano hayo mwakani nchi ya Kenya kuwa wakae tayari kwani timu kutoka Tanzania zitakuja kwenye michuano hiyo kwa kishindo.

Amesema kuwa katika mashindano ya FEASSSA mwakani ambayo yamepangwa kufanyika katika  mji wa Kakamega nchini Kenya, timu za kutoka Tanzania zitaleta upinzania mkali kwani zitakuja kwenye mashindano hayo zikiwa zimejiandaa vizuri.

“Napenda kukuhakikisha Rais wa FEASSSA kuwa tutaziandaa timu zetu vizuri ili mwakani ziweze kushinda makombe mengi,” amesema Mhe.Mwakyembe.

Aidha Mhe.Mwakyembe amezitaka timu za nchi wanachama zilizoshiriki mashindano haya kuhakikisha kuwa zinafanya maandalizi ya kutosha kwani bila hivyo zitaendelea kutofanya vizuri.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: