Mkandarasi Kasturi Flances Madange akitoa maelezo ya kina kwa Naibu waziri wa maji (wakwanza kulia ) Mhe. Jumaa Aweso wakiwa wameambatana na Mkuu wa wilaya ya Arumeru. 

Na Lucas Myovela_Arusha

Naibu waziri wa Maji Nchini Tanzania Mhe. Juma Aweso, amewataka wakandarasi hapa nchini kuwa makini na miradi ya maendeo ya wananchi kwa kufanya kazi kwa weledi na uzalendo kwa maendeleo ya nchi na ustawi wa taifa letu.

Amesema hayo wakati alipokuwa akikagua ujenzi wa mradi wa maji wa Makilenga katika tarafa ya King'ori wilayani Arumeru mkoani Arusha mradi unaojengwa chini ya serikali utakao ghalimu fedha za tanzania milioni 3.6 mpaka kukamilika kwake.

Mbali na ukaguzi huo wa mradi wa maji Awesu amempongeza kwa dhati mkandarasi huyo Bw. Kasturi Flances Madange anaye jenga mradi huo wa maji kupitia kampuni yake ya Fraju Group Ltd yenye makao yake makuuu jijini Arusha.

"Nimelidhishwa kwa dhati na mkandarsi huyu na ni kuombe Mh Dc Muro watu kama hawa ni mifano ya kuigwa na wapewe tenda ( kazi ) nyingi za miradi wananchi kwani wanfanya vizuri na kwa uzalendo mkubwa leo hii huu mradi unaenda kuondoa kero za wananchi wa kata tano na vijiji 22 ndani ya Halmashauri hii huyu mkandarasi ni mtu wa kuingwa hapa nchini na nopo tayari sasa kusaini ( kupitisha ) masai yake yote maana nimelidhishwa na utendaji kazi wake." Alisema Juma Aweso.

Mbali na ukaguzi huo wa mradi wa maji Uweso aliwataka wananchi kuvitunza vyanzo vya maji na kuvienzi ili kutopoteza asili ya maji maana ni humimu sana kwa maisha ya kila kiumbe hai na hasa binadamu ndiyo wenye uhitaji mkubwa  wa maji na kuhaidi kutowafumbia macho wanaoharibu kiundombinu ya maji.
Nae kwa upande wake Mkarandarasi anejenga mradi huo Bw.Kasturi Flances Madange ameipongeza serikali ya awamu ya tano inayo ongozwa na Rais John pombe Magufuli kwa kuwajali wakandarasi wa ndani kwa kuwapa tenda za ujenzi ya miradi ya wanachi tofauti na kipindi cha mwanzo katika uongozi uliyopita.

Pia alieleza kuwa mbali na changamoto mbali mbali zinazo wakabili wao kama kampuni ya ujenzi wameweza kuzitatua kwa karibu na kuhakikisha yote serikali itayakamilisha kwakuwa ni serikali ya watu makini na yenye kupenda maendeleo na kuhaidi kuendelea kufanya kazi zilizo tukuka kwa maslahi ya taifa la Tanzajia.

"Toka tulipo kabidhiwa kazi hii ya ujenzi wa mradi huu wa maji wa Makilenga Mimi kama mkandarasi kupitia Kampuni ya Faju Group Ltd mpaka sasa tumesha ifanya kazi hii kwa zaidi ya asilimia themanini na tano (85%) na tunaendelea vizuri kabisa na mradi huu ukitunzwa vizuri utaweza kuhudumia zaidi ya vijiji vya awali na tunazidi kubora zaidi ili uweze kunufaisha wanachi wengi." Alisema Mkandarasi huyo.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: