Thursday, 15 August 2019

Baba Mtakatifu Francis Akubali ombi la Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo kustaafu. Rasmi nafasi yake ya Askofu Mkuu Jimbo la Dar Es Salaam


Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Kardinali Polycarp Pengo ameng’atuka wadhifa huo na nafasi yake imechukuliwa na Askofu Mkuu mwandamizi, Yuda Ruwa’ichi wa Jimbo kuu la Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa ya Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu (TEC), Charles Kilima, Askofu Pengo ameng’atuka baada ya kuomba kustaafu majukumu ya kuliongoza Jimbo Kuu la Dar es Salaamombi lililoridhiwa na Baba Mtakatifu Francisko na kumteua Askofu Ruwa’ichi kushika nafasi hiyo.

Askofu Pengo ameliongoza Jimbo Kuu laDar es Salaam kwa miaka 27 tangu mwaka 1992 akimpokea Askofu Laurean Rugambwa.

No comments:

Post a Comment