Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesafiri
kwa treni ya TAZARA kutoka Jijini DSM kuelekea Kisaki Mkoani Morogoro
na baadaye atakwenda Rufiji Mkoani Pwani ambako kesho atakuwa Mgeni
Rasmi katika sherehe ya kuweka jiwe la msingi mradi wa kuzalisha umeme
katika mto Rufiji.
Kabla
ya kupanda treni, Rais Magufuli ambaye ameongozana na Mkewe Mama Janeth
Magufuli amezungumza na viongozi wa TAZARA na kuwataka kuwasilisha
mapendekezo yao juu ya hatua zinazopaswa kuchukuliwa kuboresha
usafirishaji wa mizigo na abiria kupitia TAZARA.
Rais
Magufuli amesema Serikali inatambua umuhimu wa TAZARA na haiwezi
kuiacha ikifanya kazi kwa ufanisi mdogo usiowaleta manufaa Watanzania
kama ilivyokusudiwa.
TAZARA
iliyojengwa kwa msaada kutoka China, ilianza kutoa huduma mwaka 1975 na
inamilikiwa kwa ubia wa asilimia 50 kwa 50 wa nchi ya Tanzania na
Zambia.
Reli
ya TAZARA yenye urefu wa kilometa 1,860 ina uwezo wa kusafirisha tani
Milioni 5 za mizigo kwa mwaka lakini kutokana na uwekezaji mdogo
uliosababisha upungufu mkubwa wa injini na mabehewa inasafirisha chini
ya tani laki 3 kwa mwaka.
Mkurugenzi
Mkuu wa TAZARA Bw. Bruno Chingandu na Meneja Mkuu wa TAZARA Tanzania
Fuad Abdallah wamemueleza Rais Magufuli kuwa tayari mapendekezo ya
mabadiliko ya sheria yamewasilishwa Serikalini ili kuwezesha kila nchi
kuwekeza katika TAZARA kwa lengo la kuboresha usafirishaji wa abiria na
mizigo.
Rais
Magufuli ameagiza mchakato wa kufanya marekebisho ya sheria hiyo
uharakishwe ili juhudi za kununua injini na mabehewa zifanyike haraka.
Post A Comment: