Wananchi
wa Kijiji cha Mdughuyu Kata ya Kaugeri wilayani Ikungi mkoani Singida
wakisukuma gari la Mbunge wao Elibariki Kingu wakati alipokuwa amewasili
kijijini hapo jana kufanya mkutano wa hadhara.
Mbunge
wa Jimbo la Singida Magharibi, Elibariki Kingu akizungumza na
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mdughuyu iliyopo Kata ya Kaugeri wilayani
Ikungi mkoani Singida wakati alipokuwa amewasili shuleni hapo jana
kukagua ujenzi wa madarasa na vyoo.Awali shule hiyo ilikuwa na madarasa
mawili tu lakini sasa ina madarasa manne yaliyo jengwa kwa msaada wa
mbunge huyo na Diwani.
Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi, Elibariki Kingu akikagua ujenzi wa vyoo vya Shule ya Msingi Mdughuyu.
Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi, Elibariki Kingu akicheza pamoja na waimba kwaya wa Kijiji cha Mdughuyu.
Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi, Elibariki Kingu akiwahutubia Wananchi wa Kijiji cha Mdughuyu.
Wananchi wa Kijiji cha Mdughuyu wakiwa kwenye mkutano huo.
Wasanii wakitoa burudani
Mbunge
wa Jimbo la Singida Magharibi, Elibariki Kingu, akimkabidhi fedha
mmoja wa kiongozi wa Chadema aliyehamia CCM ili akanunue sare za chama.
Mbunge
wa Jimbo la Singida Magharibi, Elibariki Kingu, akimtwisha ndoo ya
maji Mwanafunzi wa Kidato cha tatu wa Shule ya Sekondary ya Mwaru,
Faidha Jumanne kutoka katika bomba lililo jengwa shuleni hapo kwa msaada
wa mbunge huyo.
Watoto wa Kata ya Mwaru wakiwa wamepanda kwenye miti wakimsikiliza mbunge wao.
Diwani wa Kata ya Mwaru Iddi Makangale akihutubia.
Na Dotto Mwaibale, Singida
WANANCHI
wa Jimbo la Uchaguzi la Singida Magharibi wamesema wakati ukifika wa
uchaguzi wa viongozi wa Serikali za mitaa na uchaguzi mkuu utakaofanyika
mwakani wagombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais, Mbunge na Madiwani
wabaki nyumbani wasiende kufanya kampeni kwani wao watawachagua tu.
Wananchi
hao waliyasema hayo kwa nyakati tofauti jana katika mikutano ya hadhara
iliyoandaliwa na Mbunge wa Jimbo hilo Elibariki Kingu yenye lengo la
kuelezea kazi za miradi ya maendeleo zilizofanywa na Serikali ya awamu
ya tano inayoongonzwa na Rais Dkt.John Magufuli na kusimamiwa na mbunge
pamoja na madiwani.
"Mheshimiwa
Mbunge wakati ukifika wa kampeni katika uchaguzi wa viongozi wa
Serikali za mitaa na uchaguzi mkuu mwakani mbaki nyumbani msije kufanya
kampeni tutawachagua tu kwa kura nyingi kwani maendeleo mliyotuletea kwa
miaka minne mliyokuwa madarakani ni makubwa mno" alisema mkazi mmoja wa
Kijiji cha Mdughuyu Kata ya Kaugeri wilayani Ikungi mkoani Singida
aliyejitambulisha kwa jina moja la Manyama.
Manyama
alimwambia Kingu kwamba Serikali ya CCM imefanya kazi kubwa ya
kuwajengea barabara, shule na zahanati hivyo wanakila sababu ya
kuwachagua wagombea watakao simamishwa kugombea nafasi za Wenyekiti wa
Serikali za Mitaa, Urais, Ubunge na Udiwani kupitia chama hicho.
Mkazi
mwingine wa Kata ya Mwaru aliyejitambulisha kwa jina la Shija alisema
wagombea wa CCM waondoe mashaka kabisa kwani watachaguliwa wote tena
bila ya kuharibika kwa kura hata moja. Shija
alisema Serikali inayoongonzwa na Rais Dkt.Johnn Magufuli imejibu
maswali yao kwani imewapelekea maji, shule na zahanati vitu walivyokuwa
wamevikosa kwa zaidi ya miaka 50.
Akihutubia
katika mikutano iliyofanyika Mdughuyu na Kata ya Mwaru Kingu alisema
miradi hiyo yote inafanyika baada ya Rais kuzuia matumizi mabaya ya
fedha za Serikali na kuzielekeza kwenye miradi ya maendeleo ya wananchi."Kwa
kweli ninyi Wasukuma mnajua kuzaa mmetuletea huyu mwanaume Magufuli
anafanya makubwa sana hapa nchini tuzidi kumuombea" alisema Kingu.
Kingu
aliwaambia wananchi hao kuwa sasa wasubiri kupata umeme wa REA ambao
tayari Serikali imetenga fedha za kuwawekea katika vijiji vyao kwa
gharama ya sh.27,000 tu.Diwani
wa Kata ya Mwaru Iddi Makangale alisema kazi inayofanywa na Rais
Magufuli na Kingu ni ya kutukuka kwani inaonekana na wananchi wa kata
hiyo wameiona kupitia miradi ya maendeleo iliyofanyika ndio maana
wanasema wataichagua CCM kwa kura nyingi.
Katika mikutano hiyo baadhi ya wananchi waliokuwa ni wanachama wa Chadema pamoja na viongozi wao walijiunga CCM.
Post A Comment: