NA
K-VIS BLOG, TABORA NA DODOMA
MOJA ya matukio yaliyoorodheshwa kwenye kalenda
ya umoja wa Afrika (AU) yanayopaswa kutekelezwa na nchi wanachama wa umoja huo
kila mwaka ni pamoja na kushiriki shughuli mbalimbali zinazohusu Utumishi wa
Umma.
Hapa nchini siku ya utumisji wa
Umma huadhimishwa kila mwaka na mwaka
huu tayari imeanza tangu Juni 16 na kilele chake ni Juni 22, 2019, ambapo kauli
mbiu ya mwaka huu ni “Uhusiano
kati ya uwezeshaji wa vijana na usimamizi wa masuala ya uhamiaji: Kujenga
utamaduni wa Utawala Bora, matumizi ya TEHAMA na ubunifu katika utoaji wa
Huduma Jumuishi.”
MFUKO mpya wa Hifadhi ya Jamii
kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) ni miongoni mwa taasisi za umma ambazo
zimeshiriki kwa vitendo katika shughuli mbalimbali zinazohusu utumishi wa umma ambako
huko Tabora, watumishi wa PSSSF walitoka ofisini na kwenda kwenye
Shirika la masistera wa mabinti wa maria Kipalapala, kiasi cha kilomita 10
kutoka Tabora mjini ili kuwahakiki wastaafu wa Mfuko huo.
Msister
hao ambao baadhi yao ni wazee, walikuwa watumishi wa umma katika sekta
za elimu (walimu), na seka ya afya (manesi) na kutokana na umri wa
mkubwa wengine hawaweze kutok kufuata huduma nje ya makazi yao, anasema
Meenja wa PSSSF mkoa wa Tabora, Bw. Jacob Cornel Sulle.
Meneja huyo anasimulia, “Tumekuja
hapa kuwatembelea wanachama wetu kwa nia ya kuwahudumia, kuna wastaafu ni wazee
hawawezi kufika ofisini kwentu ili kuhakiki taarifa zao, hivyo tumefika hapa
ili tujiridhishe kwa kuwaona physically.”
Alisema Meneja wa PSSSF Mkoa wa Tabora, Bw. Jacob Cornel Sulle.
Aidha
wafanyakazi wa PSSSF kutoka Makao Makuu ya Mfuko huo jijini Dodoma walishiriki
kikamilifu katika kuhudumia wanachama wake kwa kusikiliza maoni yao kwa lengo
la kubaini maeneo yenye kasoro ili kuboresha huduma kwa lengo la kutoa huduma
bora “PSSSF
ni mfuko mpya, hivyo kwa mwaka huu katika maadhimisho ya wiki ya utumishi wa
umma, wakurugenzi wote wakiongozwa na viongozi wa Mfuko watawasikiliza
wanachama kwa lengo la kubaini maeneo yanayohitaji kuboreshwa kwa lengo la
kutoa huduma bora kwa wanachama wetu”, alisema Kaimu Mkurugenzi Mkuu Bi.Vupe
Ligate Bi.
Ligate alisema, Mameneja katika ofisi zote pia watasikiliza wanachama kwa lengo
la kuboresha huduma. PSSSF
ilianza kufanya kazi Agosti 1, 2018. Mfuko una ofisi Tanzania Bara pamoja na
Tanzania visiwani. Siku zote lengo la Mfuko ni kutoa huduma bora na kwa wakati
kwa wanachama wake.
Afisa
Huduma kwa Wateja, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma,
(PSSSF), Bi. Asmahan Haji, (waliyevaa hijab), akizungumza na baadhi ya
wastaafu ambao ni wanachama wa PSSSF kwenye kituo cha Shirika la masistera wa mabinti wa maria Kipalapala, Mkoani Tabora Juni 19, 2019.
Mmoja
wa wanachama wa PSSSF, (kushoto), akizungumza na ujumbe wa wafanyakazi
wa PSSSF ukiongozwa na Meneja wa Mfuko huo Mkoani Tabora, Bw. Jacob
Cornel Sulle (wapili kulia), Afisa Hudma kwa Wateja, Bi. Asmahan Haji
(watatu kulia) na Afisa Malipo, Bw. Felichism Mtenga (wakwanza kulia).
Meneja wa Mfuko huo Mkoani Tabora, Bw. Jacob Cornel Sulle akizunumza na wazee hao.
Afisa
Huduma kwa Wateja, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma,
(PSSSF), Bi. Asmahan Haji, (waliyevaa hijab), akizungumza na baadhi ya
wastaafu ambao ni wanachama wa PSSSF kwenye kituo cha Shirika la masistera wa mabinti wa maria Kipalapala, Mkoani Tabora Juni 19, 2019.
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Bi. Vupe Ligate, (kulia), akimsikiliza
mwanachama huyu wa PSSSF ofisini kwake jijini Dodoma Juni 19, 2019.
Mwanachama huyu wa PSSSF (kulia), akitoa maoni yake mbele ya mfanyakazi wa Mfuko huo makao Makuu Dodoma Juni 19, 2019.
Baada
ya kuwahudumia wanachama hawa wa PSSSF kwenye ofisi za makao makuu
Dodoma, uliwadia wakati wa kuwa na kumbukumbu ya picha ya pamoja na
viongozi wa Mfuko.
Post A Comment: