Diwani wa Viti Maalum Manispaa ya Ilala Neema Nyamgarilo akizungumza na Wanawake Wajasiriamali wa Kituo cha Taarifa na Maarifa cha Sayari gruop (Katikati)makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake Wilaya ya Ilala Sauda Adei
Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchum i Wilaya ya Ilala    Sauda Adei akikabidhi fedha Mwenyekiti wa Sayasi Nipael Joshua, kata ya Zingiziwa Manispaa Ilala leo wakati wa kukabidhi   vyeti kwa vikundi vilivyopewa mafuzo na Kituo cha Taarifa na (Katikati)Diwani wa Viti Maalum Manispaa ya Ilala Neema Nyagarilo


NA HERI SHAABAN

WANAWAKE wa Wilaya ya Ilala wa Kituo cha Taarifa na maarifa   wametakiwa kushikamana ili waweze kuwa wajasiriamali wazuri watafute masoko ya Kimataifa.

Hayo yalisemwa na mgeni rasmi, Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Wilaya ya Ilala Sauda Addey wakati wa kufunga mafunzo ya Wanawake Wajasiriamali wa Kituo cha Taarifa na Maarifa Sayari Gruop Kata ya Zingiziwa .

 "Nawaomba wanawake wa Zingiziwa wilaya ya ilala  mshikamane muwe kitu kimoja katika shughuli zenu za uzalishaji kiuchumi  msimamie masoko yenu muweze kupiga hatua katika Tanzania ya Viwanda" alisema Sauda.

Sauda aliwataka  Wanawake wa Sayari Zingiziwa  vikundi vyao pia wabuni kuanzisha viwanda vidogo vidogo vya ujasiriamali  na kutafuta  masoko.

Aliwataka wanawake kujikwamua  na kuwa na upendo  na Neema waache kubaguana.

Aidha pia alisema kiongozi yoyote akipewa dhamana na serikali  ya kuongoza watu anatakiwa kusimamia vizuri watu ambao anawaongoza na kufanya kazi kwa weledi  kwani cheo ni dhamana

Alisema mfanyakazi wa serikali anatakiwa awe chachu ya kuleta maendeleo sio kuwa chanzo cha uvunjifu wa amani.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kituo cha Taarifa na Maarifa Nipael Joshua alishukuru serikali pamoja na viongozi wa Wilaya ya Ilala na Idara ya Maendeleo ya Jamii ya Manispaa  katika mchakato wa kufanikisha kuwapatia fedha zinazopitia ngazi ya halmashauri.

 Alisema  kikundi hicho kilianzishwa mwaka 2018 kikiwa na wanachama 19 kwa sasa 76 kinajishughulisha na shughuli mbalimbali zikiwemo za kiuchumi na kijamii.

Nipael alisema Kikundi cha Sayari kinashughulika na kilimo  ,utengenezaji wa Batiki, Sabuni za maji.

Dhumuni la kuanzishwa kwake ni kujikwamua kiuchumi kwa kufanya shughuli mbalimbali za uzalishaji mali na kuacha maisha tegemezi.

Akielezea dhumuni la kituo hicho kuboresha UCHUMI wa afya na kuisaidia watoto walio katika mazingira hatarishi.

Pia kutoa elimu ya Mambo ya jinsia sambamba na kuwahudumia watoto waliokuwa katika mazingira magumu kwa mfano kwa sasa kituo hicho kina kinamuhudumia mwanamke mmoja ambaye alipokelewa akiwa na ujauzito na sasa amejifungua akiwa kituo hicho baada mwanaume kumtelekeza.

"Sisi kama Sayari kituo chetu ni cha kijamii kina shughuli nyingi zikiwemo kupinga rushwa ya ngono na kupinga utekelezaji katika JAMII "alisema Joshua.

Naye Diwani wa Viti Maalum Wanawake Manispaa ya Ilala Neema Nyangarilo aliwataka Wanawake wa Manispaa ya Ilala pia kuunda vikundi vya watu watano watano ambao wanaminiana fedha zipo za Serikali.

Diwani Neema aliwatoa hofu wananchi akiwataka changamkie fursa hiyo ya kusajili vikundi vyao ili waweze kuingia katika mchakato wa kupata mikopo hiyo ambayo inatolewa na Halmashauri ya  ya Ilala kwa Wanawake ,Vijana na Watu wenye Ulemavu
Mwisho
Share To:

msumbanews

Post A Comment: