Diwani wa Viti Maalum Manispaa ya Ilala Neema Nyamgarilo akizungumza na Wanawake Wajasiriamali wa Kituo cha Taarifa na Maarifa cha Sayari gruop (Katikati)makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake Wilaya ya Ilala Sauda Adei
Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchum i Wilaya ya Ilala Sauda Adei akikabidhi fedha Mwenyekiti wa Sayasi Nipael Joshua, kata ya Zingiziwa Manispaa Ilala leo wakati wa kukabidhi vyeti kwa vikundi vilivyopewa mafuzo na Kituo cha Taarifa na (Katikati)Diwani wa Viti Maalum Manispaa ya Ilala Neema Nyagarilo
NA HERI SHAABAN
WANAWAKE wa Wilaya ya Ilala wa Kituo cha Taarifa na maarifa wametakiwa kushikamana ili waweze kuwa wajasiriamali wazuri watafute masoko ya Kimataifa.
Hayo yalisemwa na mgeni rasmi, Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Wilaya ya Ilala Sauda Addey wakati wa kufunga mafunzo ya Wanawake Wajasiriamali wa Kituo cha Taarifa na Maarifa Sayari Gruop Kata ya Zingiziwa .
"Nawaomba wanawake wa Zingiziwa wilaya ya ilala mshikamane muwe kitu kimoja katika shughuli zenu za uzalishaji kiuchumi msimamie masoko yenu muweze kupiga hatua katika Tanzania ya Viwanda" alisema Sauda.
Sauda aliwataka Wanawake wa Sayari Zingiziwa vikundi vyao pia wabuni kuanzisha viwanda vidogo vidogo vya ujasiriamali na kutafuta masoko.
Aliwataka wanawake kujikwamua na kuwa na upendo na Neema waache kubaguana.
Aidha pia alisema kiongozi yoyote akipewa dhamana na serikali ya kuongoza watu anatakiwa kusimamia vizuri watu ambao anawaongoza na kufanya kazi kwa weledi kwani cheo ni dhamana
Alisema mfanyakazi wa serikali anatakiwa awe chachu ya kuleta maendeleo sio kuwa chanzo cha uvunjifu wa amani.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kituo cha Taarifa na Maarifa Nipael Joshua alishukuru serikali pamoja na viongozi wa Wilaya ya Ilala na Idara ya Maendeleo ya Jamii ya Manispaa katika mchakato wa kufanikisha kuwapatia fedha zinazopitia ngazi ya halmashauri.
Alisema kikundi hicho kilianzishwa mwaka 2018 kikiwa na wanachama 19 kwa sasa 76 kinajishughulisha na shughuli mbalimbali zikiwemo za kiuchumi na kijamii.
Nipael alisema Kikundi cha Sayari kinashughulika na kilimo ,utengenezaji wa Batiki, Sabuni za maji.
Dhumuni la kuanzishwa kwake ni kujikwamua kiuchumi kwa kufanya shughuli mbalimbali za uzalishaji mali na kuacha maisha tegemezi.
Akielezea dhumuni la kituo hicho kuboresha UCHUMI wa afya na kuisaidia watoto walio katika mazingira hatarishi.
Pia kutoa elimu ya Mambo ya jinsia sambamba na kuwahudumia watoto waliokuwa katika mazingira magumu kwa mfano kwa sasa kituo hicho kina kinamuhudumia mwanamke mmoja ambaye alipokelewa akiwa na ujauzito na sasa amejifungua akiwa kituo hicho baada mwanaume kumtelekeza.
"Sisi kama Sayari kituo chetu ni cha kijamii kina shughuli nyingi zikiwemo kupinga rushwa ya ngono na kupinga utekelezaji katika JAMII "alisema Joshua.
Naye Diwani wa Viti Maalum Wanawake Manispaa ya Ilala Neema Nyangarilo aliwataka Wanawake wa Manispaa ya Ilala pia kuunda vikundi vya watu watano watano ambao wanaminiana fedha zipo za Serikali.
Diwani Neema aliwatoa hofu wananchi akiwataka changamkie fursa hiyo ya kusajili vikundi vyao ili waweze kuingia katika mchakato wa kupata mikopo hiyo ambayo inatolewa na Halmashauri ya ya Ilala kwa Wanawake ,Vijana na Watu wenye Ulemavu
Mwisho

Post A Comment: