Tuesday, 11 June 2019

Diwani Msophe awasaidia wananchi wanaoishi kwenye mazingira magumu


Diwani wa Kata ya Kipunguni Mohaned Msophe akikabidhi Msaada wa kwa wananchi walio katika mazingira magumu Dar es Salaam leo,Picha na Heri Shaaban)

NA HERI SHAABAN

DIWANI wa kata ya Kipunguni Mohamed Msophe,ametoa misaada mbalimbali kwa wananchi wa kata hiyo walio katika mazingira magumu.

Misaada hiyo ametoa kwa Wajane,Walemavu,Yatima  na Watoto wa shule kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Rais mpango wa Elimu bure.

Mara baada kukabidhi misaada hiyo Diwani wa Kata ya kipunguni Manispaa ya Ilala Diwani Mohamedi Msophe alisema katika kata yake ina wakazi 57,000.

Msophe alisema katika wakazi 57,000 misaada hiyo ametoa katika makundi mbalimbali ,yatima,wajane watu na watu walio katika mazingira magumu.

Msophe alisema.
alikabidhiwa misaada mbalimbali na marafiki zake vikiwemo vyakula ,na madaftari vyote amekabidhi kwa walengwa waliokusudiwa .

Aidha alisema katika kata hiyo watu walio katika mazingira magumu ambao wanatambulika mpaka sasa wapo 3000  ofisi yake ya kata maofisa maendeleo ya Jamii inawatambua rasmi kwa ajili ya misaada mbalimbali.

Alitaja baadhi ya vitu alivyogawa siku hiyo kuwa ni Mchele,Sukari,kalam na daftari.

Wakati huohuo alielezea changamoto zilizopo kata ya kipunguni ukosefu wa shule ya Sekondari ya Kata wanafunzi wanakwenda kusoma mbali,,ukosefu wa barabara ya lami pia na Zahanati ya Kata amna ilijengwa ikaishia msingi linaitaji fedha kwa ajili ya mwendelezo.

Mwisho

No comments:

Post a comment