Sunday, 2 June 2019

Arusha DC yangara mashindano ya UMISETA Mkoa wa Arusha


Na. Elinipa Lupembe.

Halmashauri ya Arusha imeng'ara katika mashindano ya mashindano ya michezo ya Shule za Sekondari - UMISETA mwaka 2019, mkoa wa Arusha kwa kushika nafasi ya kwanza kimkoa baada ya mashindano hayo kumalizika leo.Arusha.

Halmashauri ya Arusha imeongoza mashindano hayo, baada ya kujinyakulia jumla ya  vikombe 9 kati ya 28, vilivyotolewa katika mashindano hayo, yaliyomalizika leo, kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari Ilboru wilayani Arumeru.
Akizungumza wakati wa kukabidhi Vikombe kwa washishi, Mkurugenzi mtendaji, Halmashauri ya Arusha Dkt. Willson Mahera, kwa niaba ya Katibu tawala wa Mkoa Arusha, Richard Kwite, amesema  kuwa, Serikali imeamua kurejesha michezo shuleni, ili kuibua vipaji vitakavyoongeza fursa za ajira kwa vijana nchini.

Licha ya kuwapongeza wanafunzi wote walioshiriki mashindano hayo, amewataka waliochaguliwa kuwakilisha mkoa ngazi ya taifa, kufanya mazoezi kwa bidii  na kuendeleza nidhamu michezoni ili kuweza kufanya vizuri zaidi na kurushi na ushindi wa mkoa wa Arusha. kitaifa.

"Ninawapongeza wachezaji waliofikia hatua hii, hata kama hawajapata ushindi wala kuchaguliwa kwenda ngazi ya taifa, kwa kuwa wameonesha juhudi kubwa kwa kushiriki mashindano haya ya ngazi ya mkoa, ninawataka wachezaji waliochaguliwa kufanya bidii zaidi na kuleta  Vikombe vya ushindi kwa mkoa wetu" amesema Mkurugenzi huyo.

Kwa upande wao, wachezaji kutoka timu ya Halmashauri ya Arusha .... waliochaguliwa kuwakilisha timu ya Mkoa ngazi ya taifa,  wameishukuru Serikali kupata nafasi hiyo, na kuahidi kufanya jitihada zaidi ili kuweza kufanya vizuri katika mshindano hayo.

Esau Justus maarufu kama 'Cheche' mchezaji wa mpira wa miguu, amefurahi kuchaguliwa kwenye timu ya mkoa na kushukuru timu yake kuchukua ubingwa wa mkoa na kuongeza kuwa, licha ya kuwa mashindano ngazi ya taifa ni magumu lakini amejipanga kufanya juhudi katika mazoezi na nidhamu ya michezo ili kuweza kurudi na ushindi.

"Nashukuru timu yangu imeweza kuchukua ubingwa na pia kuchaguliwa katika timu ya mkoa kuwakilisha taifa, tunaahidi kufanyavizuri katika mashindano ya kitaifa" amesema mchezaji huyo.

Mashindano hayo yaliyokuwa na lengo la kupata wachezaji 100 watakao wakilisha mkoa wa Arusha katika mashindano hayo kwa ngazi ya Taifa yatakayofanyika mkoani Mtwara.
Awali, katika mashindano hayo, halmashauri ya Arusha,  imeshika nafasi ya kwanza, ikifuatiwa na halmashauri ya Arusha Jiji, ya tatu halmashauri ya Karatu, halmashauri ya Ngorongoro ikishika nafasi ya nne, kwenye mpira wa miguu wa wavulana.

No comments:

Post a Comment