Sunday, 12 May 2019

UVISHAJI VYEO VIPYA KWA VIONGOZI WAPYA WA TANAPA KATIKA MFUMO WA JESHI USU.


Baadhi ya viongozi wapya wa jeshi-usu la uhifadhi wakila kiapo cha utii katika hafla ya kutunuku vyeo vipya kwa watendaji wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania. Halfa hiyo imefanyika katika Kituo cha Mafunzo ya jeshi-usu, Mlele mkoani Katavi.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania Jenerali Mstaafu Geogre Marwa Waitara akimvisha cheo cha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa mawasilino TANAPA  Pascal Shelutete katika hafla ya uvishaji vyeo kwa Maafisa wa TANAPA.

Kamishna wa Uhifadhi wa TANAPA Dk. Allan Kijazi akishuhudia uvishwaji wa cheo kwa Naibu Kamishna wa  Uhifadhi na Maendeleo wa TANAPA Wiliam Mwakilema unaofanywa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania TANAPA  Jenerali Mstaafu George Waitara 

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania TANAPA  Jenerali Mstaafu Geogre Marwa Waitara akimvisha cheo cha Kamishna Mwandamizi Kanda ya Kusini Dkt. Christopher  Timbuka .

Kamishna Msaidizi Huduma za Shirika Kanda ya Kusini Rukia Mkakile  akiwa kwenye ukakamavu huku akipiga saluti kama heshima baada ya kuvishwa cheo hicho na Mwenyekiti wa Bodiya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania TANAPA  Jenerali Mstaafu Geogre (Waitara hayupo pichani)

Picha ya pamoja ya Wajumbe wa  Bodi ya Wadhamini ya TANAPA na  Makamishna Wandamizi mara baada ya kuvikwa vyeo hivyo, Halfa hiyoimefanyika katika kituo cha mafunzo ya jeshi-usu Mlele mkoani Katavi.

Baadhi ya watendaji wapya wakimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania TANAPA  Jenerali Mstaafu Geogre Marwa Waitara katika  hafla ya kutunuku vyeo vipya kwa watendaji wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania  TANAPA

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya TANAPA  Generali Mstaafu Geogre Marwa Waitara akikagua gwaride la wahitimu wa mafunzo ya jeshi usu.

Wahitimu wa mafunzo ya jeshi-usu wakipita kwa mwendo wa kasi katika  gwaride la utoaji wa vyeti kwa wafanyakazi wa TANAPA, Gwaride hilo lilikaguliwa na  Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya TANAPA Jenerali Mstaafu Geogre Marwa Waitara

No comments:

Post a Comment