Wednesday, 22 May 2019

UMISSETA Ilala wakabiliwa na changamoto ya Walimu wa Michezo


Na Heri Shaaban
UMOJA wa shule za sekondari UMISSETA wilaya ya Ilala wanakabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo ubovu wa miundombunu ya viwanja vya michezo na Walimu Waliosomea.

Hayo yalisemwa Dar es Salaam jana wakati wa fainali  ya  Mashindano ya UMISSETA Wilaya ya Ilala na Ofisa Michezo wilaya ya Ilala  Nicholaus Mihayo viwanja vya Air Wing Ukonga.

Mihayo alisema changamoto kubwa katika michezo hiyo ni upatikanaji wa Walimu wa michezo  waliosomea na upatikanaji wa vifaa vya michezo.

Aidha alisema changamoto zingine   upatikanaji wa vifaa vya michezo kwa wakati wa mashindano kuanzia ngazi ya Wilaya kwenda mkoa.

 "Fainali hii ya Mashindano ya UMISSETA Wilaya ya Ilala wana michezo kutoka majimbo Mawili Ilala na Ukonga wanamichezo hao wanakutana kwa ajili ya kuunda timu ya wilaya ambayo watawakilisha katika ngazi ya mkoa yanafanyika kila mwaka mara moja" alisema Mihayo.


Alisema   mashindano ya umoja wa shule ya sekondari umisseta   yanapomalizika ngazi ya Wilaya wanachagua vipaji kwa ajili ya timu ya mkoa .

Aliongeza kuwa ngazi ya mkoa Umisseta ilala wamekuwa wakifanya vizuri zaidi na kushika nafasi ya pili miaka miwili mfululizo.

Mwisho

No comments:

Post a comment