Na Ferdinand Shayo ,Arusha.
Spika wa
Bunge la Afrika Mashariki Dr.Martin Ngoga amezitaka nchi mwanachama wa jumuiya
hiyo kutekeleza mkataba wa Malabo
unaozitaka nchi hizo kutenga asilimia 10% ya bajeti zao na kuielekeza kwenye
kilimo ili kuhakikisha upatikanaji wa chakula na kukuza uchumi kupitia kilimo.
Akizungumza
katika Mkutano Maalumu kati ya Bunge hilo na Wakulima wadogo pamoja na Asasi za
kiraia zinazojihusisha na masuala ya kilimo uliofanyika jijini Arusha ,Spika
huyo amesema kuwa nchi nyingi za EAC zimekua zikisua sua katika kutekeleza
mkataba huo hivyo wanapaswa kuutekeleza.
Aidha
amesema kuwa iwapo mkataba huo utekelezaji
utasaidia kutokomeza tatizo la udumavu na matatizo ya lishe miongoni mwa
watoto ambao ndio kizazi kinachotegemewa kwa maendeleo ya Afrika Mashariki
miaka ijayo.
Mkulima
mdogo kutoka nchini Tanzania Sophia Boke amesema kuwa changamoto iliyoko kwa
sasa wakulima wanatumia majembe ya mikono na wanakabiliwa na ukosefu wa mbegu
bora na pembejeo kwa ujumla suala ambalo linarudisha nyuma maendeleo ya kilimo.
Mwanachama
wa Shirika lisilokua la kiserikali la ESAFF ,Abdul Gea amesema kuwa fursa ya
kuhudhuria katika bunge la EALA inatoa nafasi kwao kufikisha madai ya msingi ya
wakulima na kuhakikisha mkataba wa Malabo unatekelezwa ili kuinua sekta ya
kilimo.
Post A Comment: