Tuesday, 7 May 2019

RPC Songwe afunguka tena kuhusu kijana wa CHADEMA anayedaiwa kutekwaJeshi la Polisi Mkoa wa Songwe limesema wamepokea taarifa ya kutoweka kwa Mwanachama wa CHADEMA Mdude Nyangali na sasa wapo kwenye uchunguzi wa tukio hilo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe George Kyando ameiambia Clouds TV kuwa bado jeshi hilo linaendelea na uchunguzi na kuongeza kwamba kumekuwa na matukio kama haya ya watu kusema mtu amepotea wakati mwingine inakuwa hakuna ukweli.

Kauli RPC Kyando inakuja muda mfupi baada ya CHADEMA kupitia kwa Mkurugenzi wake wa itifaki,Mawasiliano na Mambo ya nje John Mrema kulituhumu jeshi hilo kuwa linahusika na kupotea kwa Mwanachama wao

No comments:

Post a comment