Sunday, 5 May 2019

Rais Kikwete awataja wanaojua ukweli kuhusu kifo cha Dk. MengiRais Mstaafu wa Awamu ya Nne , Jakaya Mrisho Kikwete amewataka watanzania kutochanganya  maneno yanayosambazwa katika mitandao ya kijami kuhusiana na sababu za kifo cha Mwenyekiti na MKurugenzi Mkuu wa Kampuni ya IPP Media, Regnald Mengi kilichotokea Dubai.

Kikwete amesema kuwa ukweli wa sababu za kifo cha Mengi wanaoufahamu ni binti yake na mdogo wake Benjamin.

”Sisi wengine tuendelee kuwa watulivu, tuache uongo tuache kuingiza yasiyokuwepo tukaichanganya jamii, Kama kweli tunampenda Mengi haya mengine ya uongo uongo hadithi za kutunga hizi tuachane nazo, tusubiri ukweli, ukweli tutaupata. Alifariki Dubai mdogo ake Benjaini alikuwepo binti yake alikuwepo, hao ndio wana ukweli hayo mengine mnayosoma soma hayo nadhani kwa sasa yaachani tusibiri wakirudi hao nadhani watatuambia ni nini hasa kilitokea na ilikuaje mpaka kile kifo kilitokea” Amesema Kikwete mara baada ya kufika nyumbani kwa marehemu Kinondoni jijini Dar.

Aidha Rais Kikwete ameomba mazuri ya Mengi yaendelee kudumishwa kwani Mengi alikuwa ni msaada wa watu wengi.

No comments:

Post a comment