Naibu waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) akisisitiza jambo wakati akifungua kongamano la Kimataifa la kisayansi kuhusu matumizi na athari za viuatilifu kwa afya za binadamu na mazingira katika nchi za afrika kusini mwa jangwa la sahara litakalofanyika katika ukumbi wa TPRI, leo tarehe 28 Mei, 2019 Jijini Arusha.
Naibu waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) akifatilia jambo wakati wa  kongamano la Kimataifa la kisayansi kuhusu matumizi na athari za viuatilifu kwa afya za binadamu na mazingira katika nchi za afrika kusini mwa jangwa la sahara litakalofanyika katika ukumbi wa TPRI, leo tarehe 28 Mei, 2019 Jijini Arusha.
Naibu waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti na Udhibiti wa viuatilifu ukanda wa Kitropiki-TPRI Dkt Margaret Mollel wakifuatilia uwasilishaji wa mada kwenye kongamano la Kimataifa la kisayansi kuhusu matumizi na athari za viuatilifu kwa afya za binadamu na mazingira katika nchi za afrika kusini mwa jangwa la sahara litakalofanyika katika ukumbi wa TPRI, leo tarehe 28 Mei, 2019 Jijini Arusha. 
Naibu waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa kongamano la Kimataifa la kisayansi kuhusu matumizi na athari za viuatilifu kwa afya za binadamu na mazingira katika nchi za afrika kusini mwa jangwa la sahara litakalofanyika katika ukumbi wa TPRI, leo tarehe 28 Mei, 2019 Jijini Arusha.
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Arusha 220919
Taasisi ya Utafiti na Udhibiti wa viuatilifu ukanda wa Kitropiki-TPRI imekuwa kitovu cha kuunda mifumo mizuri inayosimamia na kudhibiti Biashara ya Viuatilifu.  
Zipo baadhi ya nchi za Afika kusini mwa Jangwa la sahara ambazo bado hazijatengeneza mifumo mizuri ya Kisheria na sera za kusimamia biashara za viuatilifu.
Naibu waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba ameyasema hayo leo tarehe 28 Mei, 2019 Jijini Arusha wakati akifungua kongamano la Kimataifa la kisayansi kuhusu matumizi na athari za viuatilifu kwa afya za binadamu na mazingira katika nchi za afrika kusini mwa jangwa la sahara litakalofanyika katika ukumbi wa TPRI.
Mhe Mgumba ameipongeza Taasisi hiyo ya TPRI kwa kushirikiana na wadau wengine kwa kuandaa kongamano hilo Kwani ni sehemu ya kuwajengea uwezo wadau mbalimbali ili waweze kuhakikisha kuwa Visumbufu (Pests) haviwi kikwazo  katika kutimiza azma ya serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe Rais John Pombe Magufuli ya kujenga Tanzania ya Viwanda na kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.
Alisema kuwa umuhimu wa viuatilifu katika kuzalisha mazao ni jambo la wazi na muhimu katika nchi za Ukanda wa kusini mwa Afrika na maeneo mengine duniani hivyo kongamano hilo litakuwa chachu na taswira chanya katika maendeleo ya kilimo nchini.
Alisema matumizi ya viuatilifu kwa tafsiri ya wengi ni kupata mazao mengi na hivyo mapato ya kutosha na kupata uhakika wa chakula. “Suala la madhara ya viuatilifu hivi kwa afya ya binadamu na uchafuzi wa mazingira wengi hawalipi kipaumbele na hawaoni kwamba ni tatizo. Tatizo linakuwa kubwa zaidi pale ambapo wengi wanatumia viuatilifu bila kuzingatia maelekezo ya watengenezaji” Alikaririwa Mhe Hasunga
Kadhalika alisema, Visumbufu vya mazao husababisha upotevu wa karibia ya  nusu  ya mazao katika Bara la Afrika na nchi zinazoendelea hivyo Bara la Afrika likiwa linakusudia kuzalisha chakula cha kutosha kwa ajili ya watu wake ambao wanaongezeka kwa kasi, hivyo ni lazima wakulima watumie mbinu mbalimbali za kupambana na visumbufu vya mazao.
“Ingawa viuatilifu vimeleta mafanikio makubwa sana duniani katika kupambana na visumbufu vya mazao, visumbufu vya mifugo na binadamu, pia vinasababisha madhara kwa binadamu na mazingira kwa upande mwingine” Alikaririwa Mhe Mgumba
Aidha, alisisitiza kuwa katika Bara la Afrika tatizo ni kubwa zaidi kuliko maeneo mengine duniani kutokana na uwepo wa matumizi ya viuatilifu hata vile ambavyo vimepigwa marufuku maeneo mengine duniani hivyo kuhisiwa kusababisha madhara kwa maelfu ya watu wengi.
Alisema kuwa matumizi ya viuatilifu au biashara zinazohusiana na viuatilifu zinaweza kusababisha madhara ya kiafya kwa watumiaji wa viuatilifu au kwa jamii na vile vile kusababisha uchafuzi wa mazingira pale ambapo viuatilifu havijatumika kwa njia zilizo sahihi na salama.
Tanzania kuna sheria mbili zinazoongoza katika kusimamia na kudhibiti matumizi sahihi na salama ya viuatilifu.
Sheria hizi ni sheria ya  udhibiti wa visumbufu vya mimea Namba 13 ya Mwaka 1997 (Plant Protection Act No. 13 of 1997) na kanuni zake za mwaka 1999. Na sheria ya TPRI (The TPRI Act. No. 18 of  1979).
Hata hivyo, Baadhi ya nchi za Kiafrika  zinazotumia viuatilifu kwa wingi na zenye sheria hafifu za kusimamia matumizi ya viuatilifu,  madhara ya viuatilifu ni mengi sana kutokana na usimamizi hafifu na pia kutokuwepo kwa huduma ya upimaji wa madhara ya viuatilifu katika afya ya binadamu.
MWISHO
Share To:

Post A Comment: