Sunday, 5 May 2019

Malembeka awataka Watanzania kutembelea mbuga za hifadhi za Utalii


NA HERI SHAABAN,DODOMA

MWENYEKITI wa Taasisi ya Utalii 255    Mbunge wa Mkoa wa kaskazini Unguja Angelina Malembeka  ,amewataka Watanzania  kuweka mazoea ya kutembelea hifadhi mbalimbali za Mbunga za Utalii, zilizopo Tanzania ili  waweze kujifunza Utalii wa ndani.

Mbunge Malembeka aliyasema hayo Bungeni Dodoma mwishoni mwa wiki ,  wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada kupokea wageni wake ,Wahamasishaji wa Kundi la Utalii 255 kutoka Tanzania Bara walikaribishwa       kundi la utalii  walishiriki kusikiliza kikao cha maswali na majibu Bungeni Dodoma.

Alisema ziara ya Wahamasishaji wa Utalii wa 255 Kutoka Tanzania Bara na Visiwani Zanzibar wapo katika ziara ya siku tatu ,wameanza kutembelea Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada hapo   ziara inaelekea kutembelea Mbuga ya Hifadhi ya Taifa ya Tarangile Mkoa wa Mnyara.

"Hii ni sehemu ya  kampeni ya kutangaza Utalii wa ndani ,kundi la Utalii 255 linawataka Watanzania kuweka mazoea ya kutembelea hifadhi za Taifa kuangalia mambo mbalimbali  ikiwemo wanyama kama sehemu ya kujifunza"alisema Malembeka

Alisema Utalii 255 ilianzishwa hivi karibuni,ikiwa na lengo la kuwahamasisha na kuwakumbusha Watanzania kuweza kujiwekea utaratibu wa kutembelea Hifadhi na Vivutio vya Utalii vilivyopo Nchini, Ziara hii imewashirikishaka Vijana kutoka Tanzania Bara na Visiwani Zanzibar.

 Alisema kampeni hiyo ya uhamasishaji utalii inatembelea hifadhi mbalimbali za Taifa kujifunza kisha kwenda kutangaza elimu hiyo kwa jamii wajue umuhimu wa kutembelea  utalii wa ndani

Mwisho

No comments:

Post a Comment