NA HERI SHAABAN

MKUU wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema ameagiza Jeshi la Polisi Ilala kufanya ukaguzi wa kukagua mabasi yanayobeba wanafunzi yote katika wilaya hiyo na magari mabovu yanyimwe kibali cha  kusafirisha  wanafunzi.

Mjema aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati  wa kuzindua kampeni ya kuzuia ajali kwa Wanafunzi wa Shule za Msingi wilaya hiyo kampeni  hiyo imeandaliwa na  Chama cha Michezo wa mbio za Magari Tanzania ( AAT)

"Nakuagiza Mkuu wa Usalama barabarani Ilala kuanzia leo fanya oparesheni kwa gari za wanafunzi zilizokuwa mbovu marufuku kubeba watoto wetu wa shule usitoe kibali,zinahatarisha usalama wa wanafunzi wetu ,Walimu wakuu wa shule msikubali ili katika wilaya yangu akikisha gari nzima" alisema Mjema.

Mjema alisema katika wilaya ya Ilala tukishirikiana kwa pamoja inawezekana kupunguza ajali na kampeni hiyo ilioanzishwa na AAT itafanikiwa.


Alipongenza Chama cha Michezo wa mbio za Magari Tanzania amewataka mpango huo walioanzisha uwepo wilaya nzima ya Ilala kwa shule zote sio za mijini pekeyake.

Aliwataka madereva wa magari wote kuheshimu sheria za usalama barabara ikiwemo sehemu za zebra na maeneo ya shule wanapovuka wanafunzi.

Alimwagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Jumanne Shauri kumwagiza Mhandisi wa manispaa kuweka alama za vivuko vya wanafunzi maeneo yote ya shule kwa dhumuni la kupunguza ajali pindi watoto wanafunzi wakivuka.

Pia aliagiza  askari wa Usalama barabara kuongeza viwango vya faini ambavyo wanawatoza madereva wa magari ili lengo waweze kupunguza matukio ya ajali.

"Kama  mkuu wa Wilaya hii nawajali watoto wa shule zote mafunzo wanayotoa yawepo pia katika shule zingine.


Kwa upande Mwandaaji wa shughuli hiyo Chama cha michezo za Mbio za magari Tanzania Yusuph Ghor alisema vifo vya siku Duniani 3500 katika vifo hivyo asilimia 100 vya watoto  .


Yusuph alisema taasisi ya AAT inatoa elimu ya usalama ambapo mwaka ajana walitoa elimu kwa walimu 4000  kuhusiana na usalama.

Aidha alisema shule ya kisutu katika mradi huo wamefanikiwa walimu 4000 kupewa elimu.".alisema Yusuph.

Naye Mrakibu wa Polisi  kitengo cha Elimu kwa umma Makao Mkuu ya Usalama Barabarani  Abel Swai alisema jeshi hilo lipo kwa ajili ya kupunguza ajali

Swai alisema jukumu la  jeshi hilo moja wapo ni ukaguzi wa vyombo vya moto.

Mwisho
Share To:

msumbanews

Post A Comment: