Na Ferdinand Shayo, Arusha.

Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amezindua maabara ya kisasa ya nyuklia iliko katika Tume ya Mionzi Tanzania jijini Arusha ambapo maabara hiyo itasaidia kutumia nyuklia kwa ustawi wa jamii na maendeleo ya taifa.

Majaliwa amesema kuwa maabara hiyo ni muhimu katika kuhakikisha kuwa hakuna madhara yanayotokana na matumizi ya mionzi kwa kuwa na vifaa na wataalamu waliobobea katika mionzi.

Aidha amesema kuwa Tanzania ina hazina ya tank 58.2 za nyuklia katika maeneo mbalimbali ikiwemo Namtumbo,Nachingwea,Minjingu na Songea Vijijini.

"Maabara hii ya kisasa itasaidia kuongeza mchango wa nyuklia kwenye ustawi wa jamii na maendeleo ya taifa" Alisema Majaliwa

Naibu Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto Dr.Faustine Ndugulile ambaye alimuwakilisha Waziri wa Elimu na Sayansi na Teknolojia amesema kuwa maabara hiyo ya kisasa  barani Afrika imejengwa kwa ushirikiano wa Jumuiya ya Umoja wa nchi za Ulaya na serikali ya Tanzania .

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema maabara hiyo itawawezesha Wataalu kudhibiti mionzi katika maeneo mbalimbali hususan viwanja vya ndege.

Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya Atomiki  Najat Mohammed ametaja majina ya Wafanyakazi bora ambao wamedhibiti vyanzo vya mionzi katika bidhaa na maeneo ya mipakani licha ya kushawishiwa na rushwa.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: