Tuesday, 23 April 2019

Spika Ndugai : Watu wanajificha bwana, line hii bi mkubwa nyingine nyumba ndogoSpika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amesema kuwa watu wanajificha kuwa na line nyingi kwasababu anaweza kuwa na line ya bi mkubwa na bi mdogo.

Spika Ndugai ameyasema hayo baada ya Mbunge wa Rombo,Joseph Selasini alihoji, "Watu wanajificha line hii bi mkubwa line hii nyingine nyumba ndogo, line moja tu bwana majibu tafadhali."

"Jamani bado kuna swali la nongeza hapo hapo, line moja kwa mtandao mmoja, aah kama kuna swali la nyongeza simameni ntawapa nafasi kwa hili," amesema Spika Ndugai ambaye alikuwa anacheka.

Mara kadhaa Spika Ndugai amekuwa akitania, kama anaona kuna mjadala wa jambo moto moto ambapo hata kwa hili hakuwa akimaanisha.

No comments:

Post a comment