Na Editha Edward, Tabora

Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) amekabidhi Mradi wa Matrekta 14 yenye thamani ya Shilingi  bilioni 2.5 kwa vyama vya ushirika vya mkoa huo katika hafla iliyofanyika wilayani Igunga Mkoani Tabora na kutoa onyo kwa wale watakaoenda kuyaegesha bila ya kufanyia kazi.

Mbali na vyama vya ushirika Mwanri amekabidhi Matrekta kwa watu binafisi wakiwemo mapdri, Maaskofu, na Masheikh wa mkoa huo huku akisisitiza kuwa Matrekta hayo yatumike katika Shughuli za kuleta maendeleo kwa mkoa na Taifa kwa ujumla

Pia mkuu huyo wa Mkoa mbali na kulishukuru Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC)  kwa mpango wake wa kutoa Matrekta kwa Wakulima ameliomba Shirika hilo Kuchangamkia Fursa nyingine za uwekezaji zinazopatikana katika mkoa wa Tabora

Hata hivyo mkoa wa Tabora una fursa za uwekezaji kwenye wilaya zake zote katika Sekta za  Nyama,  Asali,  Ngozi, na Tumbaku ikiongoza kwa asilimia 60 huzalishwa nchini.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: