Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka amesema Kambi za Kitaaluma mkoani Simiyu kwa wanafunzi wa darasa la saba, kidato cha nne na kidato cha Sita, ambayo ni madarasa yanayofanya Mitihani ya Taifa ya kuhitimu elimu ya Msingi na Sekondari zitakuwa endelevu.

Mtaka amesema hayo jana wakati akihitimisha Kambi ya Kitaaluma kwa wanafunzi wa kidato cha sita iliyofanyika kwa takribani mwezi mmoja katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa, ikihusisha wanafunzi 1166 kutoka katika shule 12 mkoani hapa.

Amesema Mkoa utaendelea kufanya jitihada na kuboresha zaidi kambi hizo huku akieleza kuwa ameshawaelekeza Wakurugenzi wa Halmashauri zote mkoani humo kutenga fedha kwa ajili ya motisha kwa walimu na wanafunzi watakaokuwa wakifanya vizuri.
Share To:

Post A Comment: