MCHUNGAJI Wa Mitume na Manabii Tanzania, Daudi  Komando Mashimo, amewataka wale wote wanaosema Bunge  dhaifu wafute kauli hizo badala yake wasimame na kujenga Muhimili huo  ili uheshimiwe.

Ameyasema hayo leo  Ofisini kwake Kinondoni Studio, Jijini Dar es salaam, Mara baada ya kurudi Bungeni Dodoma kufuatia mwaliko Wa Mbunge Wa Geita Vijijini, Mh Msukuma. Mchungaji Mashimo amesema lazima watu watofautishe Bunge  na wabunge kabla hawajatoa kauli za kusema.

Amesema kuwa  Bunge  sio dhaifu kama watu wanavyosema bali  kuna baadhi ya wabunge Bungeni ndio wadhaifu ambao wao  kila jambo wanapinga liwe zuri au baya.


 Amesema Bunge  ni sehemu takatifu ndio maana watu wapo pale kwa ajili ya kutunga Sheria zinazo simamia Maendeleo ya Taifa.


 Amewataka Viongozi mbali mbali hapa nchini dini na kisiasa ifike wakati Bunge liheshimiwe na kama wapo baadhi ya Viongozi wana bifu zao watafute maeneo ya kutatua sio Bungeni.


 Amesema alichokigundua Mara baada ya kutoka Bungeni ni kwamba wapo baadhi ya wabunge dhaifu na sio bunge  huku akitoa mfano Mkoa Wa Dar es salaam unawabunge wengi na wasanii wengi wapo dar lakini hakuna hata mmoja aliyesimama kuwatetea wasanii hao zaidi ni Mbunge mmoja tu kutoka Mkoa Wa Geita Vijijini ,Mh Joseph Kasheku Msukuma , kutetea wasanii na soko la  filamu.



Amesema Bungeni kuna wabunge wawili kutoka upinzani Mbunge wa  Iringa Mjini mh  Peter Msigwa na Mbea Mjini Joseph Mbilinyi  wao  wana pinga kila kitu jambo Bunge.


 Aidha Mchungaji Mashimo amewapongeza Wabunge Wa CCM kwa kusimamia hoja kwa ajili ya kujenga nchi huku akiwataka wapinzani kuacha kupinga kila jambo bila ya kuwa na hoja ya Msingi kitu ambacho kinachelewesha Maendeleo kwa Wananchi waliowaweka madarakani.

 " Unaposema Bunge ni dhaifu unachafua Bunge lote, kwahiyo yule anayedharau Bunge ambalo toka uhuru linatuongoza na linatunga Sheria sio busara na hatujengi tunaharibu " Amesema Komandoo Mashimo. 


Pia amewataka Watumishi Wa Mungu kuacha unafiki katika kuingilia mambo wasiyoyajua badala yake wao  waelekeze Nguvu katika kuliombea Taifa hili na kuombea Bunge lifanye kazi zake kwa amani.



Mbali na hayo amemtaka Mchungaji aliyesimama jina  limeifadhiwa aliyemuomba Spika Wa Bunge Mh Job Ndugai amuome radhi C.A.G atengue kauli yake Mara moja.


 Ametoa maagizo kwa Wachungaji na Manabii Tanzania watenge muda Wa wiki 2 kila mwezi kuliombea Bunge na wasipofanya hivyo ataongea na Mungu awapige kibao.


Mwisho amewapongeza baadhi ya Wabunge Wa upinzani wale wanaotetea vizuri maslahi ya Wananchi wao  bila kupinga kila jambo na kuwaombea Viongozi wote Afya ikiwamo Serikali yote ya awamu ya tano  chini ya Dkt John Magufuli.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: