Halmashauri zote nchini zimetakiwa kutokubomoa nyumba za wananchi  ambazo zipo kwenye makazi holela,ambayo hayakupimwa na badala yake  ziweke utaratibu  utakaowezesha kuwapatia hati miliki wa nyumba hizo.

Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Ardhi, nyumba na makazi, William Lukuvi  ,alipokuwa kwenye maazimisho ya siku  ya nyumba Duniani, ambayo imeandaliwa na benki ya NMB, kwa lengo la kuhamasisha wananchi  kuchangamkia fursa ya mikopo ya nymba inayotolewa na benki ya NMB.

Waziri Lukuvi,amesema serikali inatambua asilimia 70 %  ya  wananchi wanaishi kwenye makazi holela ambayo hayakupangwa hawatakiwi kubomolewa nyumba zao badala yake imeaanzisha mpango wa kurasimisha makazi yao na hivyo  wasibomolewe nyumba zao.

Amesema serikali katika kuhakikisha wananchi waisho kwenye makazi holela hawabomolewi nyumba zao  imewezesha wamiliki wa nyumba hizo ambazo hazikupimwa wapate mikopo ya pesa kutoka kwenye benki  ili wajinyanyue kiuchumi.

Lukuvi,amewataka wananchi kuwa wazalendo kwa  kupima ardhi zao  na kulipia kodi ya serikali  ambayo imepunguzwa kutoka asilimia 15% hadi kubakia asilimia 1 % tu na kuhakikisha kila anayejenga nyumba anapata hati  miliki .
Share To:

msumbanews

Post A Comment: